Chama
cha ACT- Wazalendo kitakutana Ijumaa Oktoba 20, 2017 kujadili masuala
kadhaa, likiwemo la kujizulu kwa mwenyekiti wake wa Kamati ya Kampeni na
Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Samson Mwigamba.
Mwigamba
jana Jumatatu, Oktoba 16 aliandika barua ya kujizulu uongozi na kueleza
atabaki kuwa mwanachama wa kawaida ili aweze kupata fursa ya kuwahoji
kwa matendo viongozi.
"Nimeamua
kukaa kando kwa kuwa tumekuwa hatukubaliani na baadhi ya mambo ndani ya
chama na hasa kiongozi wetu… wacha nikae pembeni niwe mwanachama ili
niwe na nafasi ya kuwahoji vizuri viongozi wetu masuala mbalimbali na
nitabaki kuwa mwanachama mwema,’’ alisema .
Akizungumzia
uamuzi huo, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema, “Nimepokea
barua yake. Tutatafakari suala hilo na masuala mengine yanayohusiana na
hayo kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi wa chama Ijumaa.”
“Ndugu
Mwigamba ataalikwa kwenye kikao hicho. Ninamshukuru sana kwa utumishi
wake uliotukuka kwenye chama na ninamtakia kila la kheri. Mchango wake
na kujitoa kwake kwa hali na mali hakutasahaulika kwenye chama chetu,”
amesema Zitto.
0 comments: