Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Selemani Jafo amekabidhi rasmi Hospitali za Rufaa za Mikoa kwa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Hatua
hiyo imekuja kufuatia pendekezo lililotolewa na Rais John Magufuli
Novemba 25 aliyetaka hospitali hizo zitolewe TAMISEMI ziwe chini ya
Wizara ya Afya ili kuweza kuwapo kwa mfanano wa sera lakini pia ugawaji
wa rasilimali watu katika hospitali hizo.
Rais
aliyasema hayo alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Kampasi ya
Mloganzila na kueleza kuwa kumekuwa na utofati mkubwa wa ugawaji wa
madaktari katika hospitali za rufaa kutokana na mgawanyo huo kufanywa na
wizara mbili tofauti.
Mbali
na Rais kuagiza hospitali hizo ziwe chini ya Wizara ya Afya ili
zisimamiwe vizuri na wataalamu na pia ameiagiza wizara hiyo kurekebisha
mgawanyo wa madaktari katika hospitali zote nchini ili kuepuka uwepo
madaktari wengi katika sehemu moja, huku maeneo mengine yakiwa na uhaba
mkubwa.
“Kuanzia
leo (Novemba 27) hospitali zote za rufaa zitakuwa chini ya Wizara ya
Afya na kwetu sisi (TAMISEMI) tutabaki na hospitali za wilaya, vituo vya
afya na zahanati pekee,” amesema Waziri Jafo.
Kuhusu
madaraka ya Waganga Wakuu wa Mikoa amesema wataendelea kuwa chini ya
TAMISEMI lakini Waganga Wafawidhi wa Hospitali watapelekwa Wizara ya
Afya.
0 comments: