Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya ziara katika
bandari ya Dar es salaam, ili kufanya ukaguzi wa magari 31 ya Jeshi hilo
ambayo Mhe. John Pombe Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi hilo
ili kurahisisha utendaji kazi
Akiwa
Bandarini IGP Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na askari wa Jeshi
hilo Kikosi cha Bandari ambapo amewataka kuhakikisha wanatimiza majukumu
yao ipasavyo pamoja na kutenda haki ikiwa ni pamoja na kutoa huduma
bora kwa wateja.
Hata
hivyo IGP amewataka Polisi wasaidizi wanaofanya kazi bandarini hapo
kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuendelea kudhibiti vitendo vya
kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.
0 comments: