Serikali
ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert
Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita.
Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka.
Uamuzi
wa kusherehekea Siku ya Taifa ya Vijana ya Robert Gabriel Mugabe kila
21 Februari ulifanywa rasmi kupitia tangazo rasmi kwenye gazeti la
serikali.
Tangazo
hilo lilichapishwa Ijumaa – siku ambayo Rais Emmerson Mnangagwa
aliapishwa kuwa rais, na kufikisha kikomo uongozi wa Mugabe wa miaka 37.
Serikali
ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa
sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa
vijana katika chama cha Zanu-PF.
Bw
Mugabe aliondolewa mamlakani wiki iliyopita kutokana na shinikizo
kutoka kwa wanajeshi waliokuwa wamechukua udhibiti wa serikali wiki
iliyotangulia.
Credit:BBC
0 comments: