Watu watano wamefariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Hiace
kugongana na lori kisha kuwaka moto katika Kijiji cha Kyamyorwa wilayani
Muleba mkoani Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi amesema ajali hiyo imetokea leo Ijumaa Oktoba 20, saa 12:00 asubuhi.
Amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.
Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliopoteza maisha, Mkuu wa Wilaya ya
Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo,
kondakta na abiria watatu.
Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka.
0 comments: