Mkazi
wa jijini Dar es Salaam, Robert Massawe (51), ambaye polisi wanadai ni
mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu
wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake.
Kabla
ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa huyo anadaiwa
alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa maeneo
mbalimbali na laini za simu 58.
Taarifa
iliyotolewa jana Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,
Hamisi Issah imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa
kuamkia jana wilayani Rombo.
Alisema
mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar es Salaam na baada ya
kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi aliyoshiriki na
alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki.
Polisi
imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa Moshi na moja alikuwa
akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam.
Kamanda
Issah alisema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa kufanya tukio la
ujambazi katika Kijiji cha Chilio, Kata ya Holili wilayani Rombo jana
alfajiri.
Alisema
askari walifuatana naye chini ya ulinzi hadi Moshi kwenye dampo
lililopo jirani na kiwanda cha ngozi ambako bunduki ilifukiwa ardhini
ikiwa na risasi 24.
“Chini ya ulinzi wa askari kanzu, alipowaona wenzake alipiga kelele kuwajulisha polisi walikuwepo eneo hilo,” alisema.
Kamanda
Issah alisema kelele ziliwafanya watuhumiwa hao kukimbia huku
wakifyatua risasi hovyo na baadhi zilimpiga Massawe mkono wa kushoto,
mgongoni na mguuni hivyo kusababisha kifo chake.
Polisi
imesema mtuhumiwa alishiriki matukio manane ya uporaji wa fedha na
mauaji kwa kutumia silaha na amewahi kufungwa kwa ujambazi lakini
aliachiwa baada ya kukata rufaa.
0 comments: