Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi tawi la bokorani amejitokeza na kutoa mtizamo wake juu ya swala zima la mchakato wa katiba mpya
JOSEPH YONA ambae amenukuliwa na baadhi ya wana siasa kwamba amejitoa kimasomaso maso kuongea ukweli na kuulani unafiki alisema
👉Mimi YONA nilikuwa sifikirii somo lá History O-level Lakini nilipata "B" na kuwa Mwanafunzi pekee darasani kuwa na ufaulu huo sababu nilijikita katika mifano kila Swali nililo lijibu niliweka na mifano wake.
Sasa KATIBA na UKATIBA ni nini?
👉Wananchi wanataka Yale yoote yaliyomo kwenye katiba viongozi wetu wayaishi,Unaweza kuwa na katiba nzuri tu na Unaweza kuwa na Wapinzani wanaihubiri jukwanaani kila kukicha Yale yaliyomo kwenye katiba,mfano:-
Mh Mbowe anahubiri viongozi kukalia nyumba za serikali bure,Lakini yeye hayaishi anayohubiri anakalia jengo lá NHC zamani bilcanas bila kulipa hii si kuyaishi ya kwenye katiba.
👉Sasa Mbowe asingekuwa anahubiri maneno ya makaratasi Yaani moyoni Angekuwa na Yale yaliyomo kwenye makaratasi asingeishi jengo Lile anafanyia biashara za madawa ya kulevya,na magazeti yake.
Lakini Pia wapinzani wamekuwa kipaumbele kupiga kelele na na kusema Tanzania hakuna Demokrasia Akiwaongoza kiongozi wao wa Kambi ya Upinzani Mh Mbowe
lakini ikumbukwe CHADEMA ndio chama pekee amabacho hakina uchaguzi wa haki wa ndani ya chama Ni mbowe pekee mwenye haki ya kuongoza Chadema kwa kipindi chote cha uhai wake
ndio maaana utaona wale wote wenye akili timamu waondoka chadema
Katiba ni chombo Muhimu sana katika nchi yetu hatuwezi ruhusu watu wasio na utashi na mapenzi na Taifa letu kupandikiza Mbegu mbaya zitakazo kuja kuliathili Taifa
Walipiga kelele kuhusu kunyonywa kwenye secta ya madini toka JPM akiwa waziri sasa amenyosha ana anaendelea kinyosha usawa unapatikana wanaona watakosa la kuongea wanaungana na wazungu kupambana na serikali yetu ila hawata weza
Mwenyekiti huyo aliwataka wananchi wote na wanasiasa wa vyama vyote
Kwa sasa tujikite katika kufanya kazi Rais na Taasisi yake na watendaji wake wenye mapenzi na taifa wataendelea kugusa sehemu Muhimu zenye Tunu ya Taifa ili kuhakikisha rasilimali zetu hazipotei
pia tuache kuishi kwa mihemuko watanzania tusikubali kuwa chambo kwa wanasiasa wanao taka kututumia ili wafanikishe yale wanayo ya kusuduia ndani ya taifa letu
maelfu ya watanzania hawana uhitaji na katiba mpya ila wanauhitaji na barabara za kusafilisha mazao yao baaada ya kumaliza kuvuna kupeleka sokoni wanauhitaji na shule za kisasa na waalimu wakutosha kwaajili ya watoto wao wana uhitaji na hospitali za kiasasa na Madactari wa kutosha kwaajiri ya afya zao wanauhitaji na vitu vingi vinavyogusa maisha yao ya kila siku
NAKUOMBA RAIS WANGU
Timiza majukumu yako watanzania wengi wapo nyuma yako walala hoi wapo nyuma yako maskini wapo nyuma yako wakulima na wale wote wenye kulipenda Taifa hili kwa moyo wote wapo nyuma yako na mimi JOSEPH YONA niliye kufa na kufufuliwa sababu ya kuusemea ukweli nipo nyuma yako
ila matajiri wakorofi wa kwepa kodi wala rushwa mafisadi ndio amabao wanao kupinga na kukuzulia maneno kila kukicha
Naomba uwapuuzi na endelea na kazi zako ili ukifika mwa Mungu ukakabidhi hesabu zako kwa yale uliyo ya tenda
NI
JOSEPH YONA
Mwenyekiti wa ccm tawi la bokorani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: