Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana wa UVCCM Taifa Shaka Hamidu,
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli
kwa kurejesha mwamko ndani ya chama.
Shaka
amesema kuwa katika uongozi wa Rais Magufuli kama Mwenyekiti wa Chama
cha CCM, UVCCM imeweka rekodi ya kupokea maombi mengi zaidi ya watu
wanaowania nafasi ya Uenyekiti Taifa kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Jumla
ya vijana 113 kutoka Tanzania bara na Zanzibar wamejitokeza kuwania
nafasi hiyo.
“Katika
uongozi wa Dkt, Magufuli akiwa Mwenyekiti wa chama limekuwa ni jambo la
historia inaonyesha jinsi gani vijana wamekuwa na mwamko na hamu ya
kukitumikia chama, kwakweli anastahili pongezi na hizi ni dalili nzuri
kwa Chama”, amesema Shaka.
Kwa
upande mwingine Shaka amesema hivi sasa zoezi linaloendelea ni usaili
wa wagombea wote walioonesha nia ya kuwania uongozi ili kuwabaini na
kuwapitisha wenye sifa sitahiki. Moja ya sifa kuu ya kugombea uongozi
ndani ya UVCCM ni kuwa na miaka 30 au chini ya hapo ili katika uongozi
wako usizidi miaka 35 kwani kila awamu ni miaka mitano.
Nafasi
zinazowaniwa katika uchaguzi huo ambao mchakato wake umeanza tangu
mwezi April kwa ngazi za Shina na Tawi ni Mwenyekiti, na Makamu wake,
Wajumbe watano wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC), wajumbe watano wa
baraza kuu la umoja huo Taifa na wawakilisha wa Jumuiya hiyo katika
Jumuiya nyingine ndani ya chama.

0 comments: