Ikiwa
imebakia siku moja kuanza kusikilizwa tena kwa kesi ya mauaji ambayo
inamkabili, msanii Elizabeth Michael (Lulu) amesema yupo tayari
kukabiliana na kesi hiyo, ambayo alijua ipo siku itarudi tena.
Lulu
ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio,
na kusema kuwa alikuwa na taarifa ya kesi hiyo kabla watu hawajaipata
kwenye mitandao, na utaratibu wa kisheria ulifuatwa.
“Unajua
watu hawajui sheria, kesi haikuwahi kuisha ni pocedure ya kawaida ya
mahakama imefuatwa na ni muda wake umefika sasa , siyo kama imeibuka tu,
na kwasababu mimi ndiye muhusika nimepata taarifa kwa njia ya kisheria
siyo kama nyie kwenye mitandao, na pengine niliipata kabla yenu”,
amesema Lulu.
Lulu ameendelea kusema kwamba kuwepo kwa kesi hiyo kunamuathiri kwa kiasi kikubwa kwenye kazi zake na maisha yake kiujumla.
Kesi
inayomkabili muigizaji huyo wa bongo movie inatarajia kusikilizwa tena
kesho Oktoba 19, 2017 baada ya kuwa nje kwa dhamana kwa muda mrefu.
Elizabeth
Michael (Lulu) anakabiliwa na kesi ya kusababisha kifo bila kukusudia
cha aliyewahi kuwa muigizaji wa filamu nchini, Steven Kanumba, mnamo
April 7, 2012 .
0 comments: