Afisa
Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi
amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na kosa la kumiliki mali ambazo ni magari 19 na kuishi
maisha ya kifahari kinyume na mshahara wake
Mshtakiwa
amesomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na
Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambaye alidai mshtakiwa ana makosa
mawili.
Alidai
kuwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya
Jiji la Dar es Salaam, akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Afisa Msaidizi wa
Forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume
na sheria.
Inadaiwa
kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akimiliki magari 19 ambayo ni Toyota RAV4,
Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry,Toyota Ipsum, Toyota
Wish,Toyota Mark ll, Toyota Regiusage, Toyota Estima, Toyota Alex,
Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Lasso,
Suzuki Carry, ambayo yana thamani ya Tsh. Milioni 197.6.
Kosa
la pili, anadaiwa kuwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 jijini
Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu
yenye thamani ya Tsh. 333,255,556.24 tofauti na kipato chake.
Wakili
Peter amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo anaomba
Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali
(PH).
Hata
hivyo, upande wa utetezi kupitia Wakili Elisalia Mosha aliiomba
Mahakama hiyo kumpa dhamana mteja wake kwa sababu mashtaka aliyonayo
yanadhaminiika kisheria.
Hakimu
Shaidi alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya
Tsh. Milioni 20 ambapo alikidhi masharti na kuachiwa huru kwa dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Novemba 7, 2017.
0 comments: