Kesi
ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa fani ya uigizaji filamu
nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu imeahirishwa hadi kesho Jumatano
Oktoba 25,2017.
Kuahirishwa
kwa kesi hiyo leo Jumanne Oktoba 24,2017 kunatokana na Jaji Sam
Rumanyika kuamuru polisi aliyechukua maelezo ya shahidi Josephine
Mushumbusi kufika mahakamani.
Awali,
Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lulu katika kesi hiyo aliieleza
Mahakama Kuu kuwa shahidi huyo hapatikani kwa kuwa yuko nchini Canada.
Kibatala aliiomba Mahakama iyapokee maelezo yake kama sehemu ya ushahidi.
Wakili
wa Serikali, Faraja George alisema hapingi kuwasilishwa maelezo hayo
mahakamani, bali anapinga kuwasilishwa na wakili Kibatala kwa kuwa yeye
si aliyeyaandika.
Shahidi
huyo ni wa pili wa upande wa utetezi baada ya Lulu kujitetea jana
Jumatatu Oktoba 23,2017. Alijitetea baada ya Jaji Rumanyika kusema ana
kesi ya kujibu.
Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa filamu, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012, nyumbani kwa marehemu Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
0 comments: