Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewapiga marufuku askari wa kikosi
cha FFU na kusema hataki kuwaona wakisumbua wananchi katika eneo la
Ukonga Dar es Salaam na kutaka waliohusika wachukuliwe hatua kwa kitendo
walichofanya kuwapiga wananchi.
Sophia
Mjema amesema hayo alipowatembelea wananchi hao ambao wamelalamika
kufanyiwa fujo na kupigwa na askari hao kwa siku mbili kutokana na
askari mmoja kuuwawa na watu wasiojulikana.
Mkuu
wa Wilaya anasema kuwa askari hao walipaswa kufanya uchunguzi kujua ni
watu gani walihusika kufanya mauaji ya askari huyo na si kwenda kufanya
fujo na kuwapiga wananchi pasipokuwa na sababu.
"Kama
kuna askari alipatikana ameshafariki utaratibu ulikuwa uchunguzi
ufanyike ili waweze kujiridhisha baada ya hapo wale ambao wangetambulika
ndiyo wangechukuliwa hatua lakini kwa hili halikubaliki, kwa hiyo
nasema hivi askari wote waliohusika kufanya fujo na vurugu wachukuliwe
hatua za kinidhamu na huku barabarani sitaki kuona FFU yoyote anasumbua
wananchi" alisema Mjema
Aidha
Mkuu wa Wilaya huyo ametaka wananchi ambao wameumizwa na askari hao kwa
vipigo kwa siku mbili mfululizo waweze kujiorodhesha kwa majina ili
wapatiwe matibabu na kusema wale ambao wamepoteza mali zao utaratibu
utafanyika kuona nini kifanyike
0 comments: