Abiria
hao waliokaa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa nne kuanzia saa 3:00
asubuhi walipotakiwa kusafiri hadi saa 7:00 mchana, walianzisha vurugu
kushinikiza kupatiwa usafiri.
Akizungumzia
kadhia hiyo, Meneja wa FastJet Mkoa wa Mwanza, Ezekiel Manyiga amesema
ndege iliyotakiwa kusafirisha abiria hao haikufika kutoka jijini Dar es
Salaam kutokana na kupata hitilafu ya kiufundi.
“Hata
abiria waliotakiwa kusafiri kutoka Dar es Salaam kuja Mwanza hawajafika
hadi sasa; tunafanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kutatua tatizo
hili,” amesema Manyiga
Ilipofika
saa 7:00 mchana jana, uongozi wa kampuni hiyo ulifikia uamuzi wa
kuwarejeshea nauli abiria waliokuwa tayari kupokea fedha zao ili
kutafuta usafiri mwingine pamoja na Sh30, 000 ya kujikimu kwa kila
abiria aliyekosa usafiri.
“Watakaokuwa tayari kusubiri ndege yetu watalazimika kusafiri kesho (Jumatano) kwa sababu ndege tayari imejaa,” amesema Manyiga
0 comments: