Mrembo
anayeshikilia Taji la Miss Tanzania 2016/17, Diana Edward amenusurika
kukeketwa na ndugu zake nyumbani kwao, Sakina jijini Arusha.
Akizungumza
na Ijumaa mapema wiki hii akiwa katika mazungumzo na warembo waliokuwa
wakishiriki kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Ubungo 2017 yaliyofanyika
Ukumbi wa JBN, Kijitonyama jijini Dar, Diana ambaye kiasili ni Mmasai
alisema kuwa, tukio hilo hatalisahau kwa kuwa alifanikiwa kuchoropoka
mikononi mwa ndugu zake hao waliotaka kuhakikisha anafanyiwa tohara hiyo
kama wenzake. “Kwa mila za kwetu mwanamke ukifikia umri fulani ni
lazima afanyiwe ukeketaji.
Kwangu
mimi sikutaka kabisa kitu kama hicho kinitokee lakini kitendo cha kutia
mguu nyumbani kwetu hivi karibuni huko Sakina, ndugu pamoja na watu
wengine walinifuata na kunitaka nikeketwe, kisa kutimiza mila.
“Hata
hivyo, nilifanikiwa kutoka mikononi mwao japokuwa hadi sasa hivi bado
kuna ndugu wanaendelea kushikilia msimamo wa mimi kufanyiwa hivyo,
lakini mwisho wa yote sikukubali kufanyiwa mambo yaliyopitwa na wakati,”
alisema Diana huku akilengwa na machozi. Diana alikuwa Miss Tanzania
mwaka jana katika kinyang’anyiro kilichofanyika jijini Mwanza
akiwakilisha Wilaya ya Kinondoni.
0 comments: