Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya mawaziri na kuwataka watumie madaraka
yao kwa manufaa ya Taifa na kamwe wasiyatumie kama fursa ya
kujitajirisha wao binafsi.
Kassim
Majaliwa amesema hayo leo Oktoba 16, 2017 alipozungumza na baadhi ya
Mawaziri, Manaibu na Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika jijini
Dar es Salaam.
Aidha
Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza
kwamba amewateua ili wafanye kazi na kamwe wasitumie madaraka waliyopewa
kwa maslahi yao binafsi.
“Madaraka
haya ya Uwaziri si fursa ya kujipatia utajiri, tunatakiwa tufanye kazi
kwa weledi, uadilifu, bidii na uaminifu mkubwa ili kuondoa kero za
wananchi kwa wakati.”
Waziri
Mkuu amesema Mawaziri hao wanatakiwa wasimamie utekelezaji wa mpango wa
maendeleo wa Taifa wa miaka kuanzia mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021. Pia
utekelezaji wa ahadi zote zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2015 pamoja na ahadi alizozitoa Rais Dkt Magufuli wakati wa
kampeni za uchaguzi.
Hata
hivyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri hao wakapunguze urasimu katika
utekelezaji wa malengo ya Serikali kwa sababu wananchi wanahitaji
kuhudumiwa kwa wakati
Mawaziri
waliohudhuria kikao hicho ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Bw.
Suileiman Jaffo pamoja na Manaibu wake Bw. Joseph Kandege na Bw. George
Kakunda, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi
Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Faustine Ndungulile.
Wengine
ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu wake
Bw. Jumaa Aweso, Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Charles Mwijabe na
Naibu wake Mhandisi Stella Manyanya.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Naibu wake Bw.
Josephat Hasunga, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako na Naibu wake Bw. William Ole Nasha, Naibu waziri wa Mifugo
na Uvuvi Bw. Abdallah Ulega pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara hizo.
0 comments: