Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya uteuzi wa majina ya wagombea wa uenyekiti wa wilaya sita za kichama.
Wilaya hizo ni Moshi Mjini, Hai, Siha, Makete, Musoma Mjini na Musoma Vijijini.
Taarifa
kwa umma iliyotolewa na CCM jana Jumatatu Novemba 20,2017 imesema
Kamati Kuu ya chama hicho kwa niaba ya Halmashauri Kuu imeteua majina ya
wagombea katika wilaya ya Hai ambayo ni ya Abdulah Mriri, Magai Maganda
na Justice Masawe.
Kwa
Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro walioteuliwa ni Justice Mkita,
Wilfred Mossi na Humfrey Nnko, huku Wilaya ya Moshi Mjini wateule ni
Absalom Mwakyoma, Joseph Mtui, Faraji Swai na Alhaji Omar Amin Shamba.
Taarifa
hiyo iliyosainiwa na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Humphrey
Polepole imesema kwa Wilaya ya Makete wateule ni Aida Chengula, Mwawite
Njajilo na Onna Nkwama; Wilaya ya Musoma Mjini ni Robert Sylvester,
Magiri Maregesi, Amina Nyamgambwa na Daud Misango.
CCM imesema wateule wa Musoma Vijijini ni Gerald Kasonyi, Kananda Hamisi Kananda na Nyabukika Bwire Nyabukika.
Polepole
katika taarifa hiyo amesema Kamati Kuu imeagiza mikutano mikuu ya
uchaguzi ya wilaya za Makete, Musoma Vijijini na Musoma Mjini ifanyike
Novemba 25 na 26,2017.
Kwa wilaya za Moshi Mjini, Hai na Siha mikutano hiyo itafanyika Desemba Mosi na 2, 2017.
0 comments: