Serikali imesema itaendesha msako na kuvifunga vyuo vyote vya afya visivyokidhi vigezo na msharti ya uwepo wake.
Hayo
yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, alipozungumza
kwenye mahafali ya Chuo cha Tiba na Afya cha KAM.
Alisema
ingawa ni kweli kuna uhaba mkubwa wa watumishi wa sekta ya afya, lakini
serikali haiwezi kuvumilia vyuo ambavyo vinajiendesha bila kufuata
miongozo ya serikali.
“Ni
kweli tuna uhaba wa watumishi zaidi ya 95,000 wa sekta ya afya lakini
hakiwezi kuwa kigezo cha watu kujiendesha kwa ubabaishaji ubabaishaji,
lazima miongozo ifuatwe,” Mh. Ndugulile.
Aidha,
waziri huyo alisema serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa
unaotolewa na vyuo binafsi hivyo itaendelea kushirikiana navyo kutatua
changamoto mbalimbali ili viweze kustawi na kutoa wahitimu wengi zaidi
watakaosaidia taifa.
It has turned to be as business as usual God forbid.
ReplyDeleteIt has turned to be as business as usual God forbid.
ReplyDelete