Ongezeko la shughuli za kibindamu na viwanda kwa ujumla
imesababisha kuongezeka kwa hewa ya ukaa na majanga yatokanayo na
mabadiliko ya tabia nchi mfano mafuriko na joto kali ambalo husababisha
magonjwa na athari kwa viumbe hai na binadamu kwa ujumla hasa katika
miji mikubwa ikiwemo jiji la Dar es salaam.
Katika
kutekeleza na kuunga mkono kampeni ya utunzaji wa mazingira maarufu
kama “mti wangu” iliyozinduliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es saalam , Mh
Paul Makonda, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na
wafanyakazi wake leo imeshiriki katika kupanda majani , miti na kuweka
mbolea ili kutunza mazingira na kuyaweka katika hali ya kuvutia
Bustani
hiyo inayoanzia katika mataa ya Moroco hadi maeneo ya mgahawa wa Best
Bite katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi ilikabidhiwa kwa kampuni ya
Airtel na mh. Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kuboresha na kutunza mazingira
ya jiji la Dar es saalam
Ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa kampeni hii, leo wafanyakazi wa Airtel kwa kushirikiana
na serikali tunashirikia katika zoezi la kupanda majani na miti katika
eneo la katikati ya barabara. Airtel tunaamini ili tuweze kufanya
biashara tunahitaji mazingira bora na kwa kupitia kampeni hii ya mti
wangu tunaunga mkono juhudi hizo kwa kuyatunza mazingira
yanayotuzunguka na kuyaweka katika hali ya usafi na kuvutia” alisema
Airtel Afisa Mazinga wa Airtel ,Bwana Ncheye Mazoya
Kwa
upande wake Afisa Mazingira wa wilaya ya Kinondoni, Bwn Awadhi
Kinajambo alisema “tunatoa shukurani kwa kampuni ya Airtel kwa kuunga
mkono jitihada hizi za kutunza mazingira kupitia kampeni hii mahususi ya
“Mti Wangu”. Tunaanmini juhudi hizi zitasaidia katika kuboresha hali
hewa,kuondoa tishio la majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi
pamoja na kupendezsha jiji letu la Dar es salaam”.
Natoa
wito kwa wakazi na wafanyabiashara wa maeneo haya kutokatiza kwenye
bustani hii wala kutupa taka ili tuweze kuunga mkono kwa vitengo zoezi
hili kuwa la mafanikio na kwa pamoja kutunza mazingara yetu.
Afisa
Mazingira wa Airtel, Ncheye Mazoya akimwagilia mti baada ya kuupanda,
wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliposhiriki kupanda majani, miti
na kuweka mbolea katika bustani iliyopo katika Barabara ya Ali Hassan
Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es Salaam jana, kuunga
mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama “mti wangu”,
iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda. Kushoto
ni Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kinondoni, Awadh Jambo.
Wafanyakazi
wa Airtel wakishiriki kupanda miti katika bustani iliyopo katika
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es
Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama
“mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul
Makonda.
Wafanyakazi
wa Airtel wakishiriki kupanda majani katika bustani iliyopo katika
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es
Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama
“mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul
Makonda.
Wafanyakazi
wa Airtel wakishiriki kupanda majani katika bustani iliyopo katika
Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kuanzia Moroco hadi Namanga jijini Dar es
Salaam jana, kuunga mkono kampeni ya utunzaji mazingira maarufu kama
“mti wangu”, iliyozinduliwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo, Paul
Makonda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: