Bad News: MKE AUA MME WAKE KWA KUMCHINJA HUKO TINDE SHNYANGA
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule
****
Habari
zilizotufikia kutoka katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga zinasema
mwanamke aliyejulikana kwa jina la Mama Tatu amemuua mme wake
anayejulikana kwa jina la “Mzaramo” kwa kumchinja kisu shingoni na
kumchoma kisu tumboni.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Alhamis Septemba 21,2017 katika eneo la Malenge/Uswahilini kata ya Tinde.
Inaelezwa
kuwa wanandoa hao walikuwa wamegombana,ndipo mke akamsubiri mmewe alale
na alipolala akamchoma kisu tumboni na shingoni.
“Baada ya
kutekeleza tukio hilo,mwanamke huyo alifungua radio kwa sauti ya juu
kisha kumfunga mlango kwa kufuli kisha kukimbilia Shinyanga Mjini ambapo
kuna Mama yake mzazi,alipofika akamwambia mama kuwa amefanya
mauaji,hali iliyomfanya mama atoe taarifa polisi na kufanikisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa”,mashuhuda wameiambia Malunde1 blog
“Wanandoa
hawa wamepanga nyumbani kwa Kaboja,mme huwa anaonekana mara moja moja
hapa Tinde kwa sababu anafanya kazi katika mgodi huko mkoani
Geita”,wameeleza mashuhuda wa tukio hilo.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Simon Haule amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Taarifa kamili tutawaletea hivi punde....
0 comments: