SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI YA UALIMU WA SHULE YA MSINGI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetangaza ajira
za walimu wa shule za msingi kwa walimu ambao wamemaliza masomo yao
mwaka 2014/2015 katika ngazi ya cheti (III A).
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu
Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kuthibitishwa na Msemaji
Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas imesema kuwa walimu ambao wamemaliza
mwaka 2014/2015 na walituma maombi yao kwenye tangazo la kazi ya Agust
10, 2017 hawatakiwa kuomba upya kwani barua zao zinafanyiwa kazi.
0 comments: