JITIHADA ZA KUMPELEK TUNDU LISSU ZAGONGA MWAMBA
Mbunge
wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambaye amekuwa akifuatilia kwa
ukaribu matibabu ya mbunge mwenzake wa Singida Mashariki Tundu Lissu,
ameweka wazi kwamba jitihada za kumpeleka Lissu Marekani kutibiwa kwa
sasa zimegonga mwamba.
Lazaro
Nyalandu ametoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook ambapo
amendika ujumbe kuhusu kauli ya madaktari wanaomtibu Tundu Lissu jijini
Nairobi Kenya, na kueleza kwamba madaktari hao wamesema hawawezi
kuruhusu Tundu Lissu asafirishwe kupelekwa Marekani kutokana na hali
yake jinsi ilivyo.
“Kwa
sasa mipango ya kumsafirisha Mheshimiwa Tundu Lissu nje itasimama
kutokana na ushauri wa madaktari wa hospitali ya Nairobi, ili kuruhusu
kukamilishiwa huduma za tiba ambazo tayari ameanzishiwa hadi hapo
itakavyoshauriwa au vinginevyo, ama endapo kutatokea umuhimu wa kufanya
hivyo katika siku zijazo”, ameandika Lazaro Nyalandu.
Hapo
jana Lazaro Nyalandu alitoa taarifa kwamba wanafanya jitihada za
kumpeleka Tundu Lissu Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi, huku
wakisubiria ripoti ya madaktari wa hospitali ya Nairobi ambako mbunge
huyo anatibiwa, na ndipo ilipokuja taarifa hiyo kwamba haitowezekana
kumsafirisha kwa sasa.
Ikumbukwe
kuwa Mbunge Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba
7, 2017 mjini Dodoma majira ya mchana, na usiku wa siku hiyo hiyo
alikimbizwa jijini Nairobi kwa ajili ya matibabu zaidi, kutokana na hali
yake kutokuwa nzuri.
==>>Huu ni ujumbe alioundika Lazaro Nyalandu
TUNAFAHAMU
kwamba, tangu Alhamisi, Septemba 7, siku ambayo Mh #TunduLissu, Mb.,
(Singida Mashariki-CHADEMA) alishambuliwa kwa kupigwa risasi mjini
DODOMA, Watanzania wengi wamesononeshwa na kulia sana, na kubwa zaidi,
WOTE wameungana katika kuomba Sala na Dua kwa ajili ya Mh #TunduLissu,
ili mkono wa Mkombozi, aliye MUNGU wetu, upate kumgusa tena na kumponya
dhidi ya majeraha, maumivu na mateso anayoyapitia.
MAPEMA leo, baada ya kutembelea #NairobiHospital asubuhi, nimefanya
mazungumzo mchana wa leo na Mh #FreemanMbowe, ambapo kwa pamoja
tumeelezwa kuwa MADAKTARI #NairobiHospital wameendelea na kumtibu Mh
#TunduLissu, ikiwa ni pamoja na kuanza upasuaji, na huduma zingine za
Kitabibu walizomwanzishia tangu awasili Nairobi siku ya Alhamisi,
Septemba 7. IMEELEZWA vilevile kuwa kwa sasa Mh #TunduLissu ataendelea
na TIBA hospitalini hapo kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hali yake
bado ni "Critical but stable", na KWAMBA mwili wake unaendelea kuitikia
vema matibabu lukuki anayofanyiwa kwa wakati mmoja.
KWA SASA, mipango ya kumsafirisha Mh #TunduLissu NJE itasimama, kutokana
na ushauri wa MADAKTARI #NairobiHospital, ili kuruhusu kukamilishiwa
huduma za TIBA ambazo tayari ameanzishiwa, hadi hapo itakavyoshauriwa
vinginevyo, ama endapo kutatokea umuhimu wa kufanya hivyo katika SIKU
zijazo.
AIDHA, SOTE tuzidi KUMWOMBEA MUNGU na kushiriki katika CHANGIZO za kusaidia gharama za matibabu yake.
NI DHAHIRI kwamba Wana Singida, na Watanzania WOTE tumeumia, tumekwazwa,
na tumesononeshwa sana kwa uonevu na dhuluma aliyotendewa ndugu yetu Mh
#TunduLissu. Kitendo hiki hakikubaliki mbele za MUNGU na mbele za
wanadamu.
Tunaiomba Serikali yetu iendeleze juhudi zake na kuchukua hatua za
haraka kuwasaka, kuwakamata, na kuwatia mbaroni watu wote waliohusika
kupanga na kutekeleza shambulio hili la kigaidi dhidi ya Mh #TunduLissu.
Aidha, shambulio hilo walilolifanya watu wasiojulikana limedhalilisha
taifa, na kudhoofisha taswira ya kukomaa kwa demokrasia inayoruhusu
kuvumiliana na kuheshimiana licha ya tofauti zetu za kiitikadi na
mitazamo ya kisiasa.
HALIKADHALIKA, kwetu sote kama TAIFA, huu ni wakati wa Watanzania wote
kuwa wamoja, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi, kidini, wala
kikabila, tuungane na kulaani kitendo hiki na vitendo vyote vya uonevu
na kuumizana. TANGU zamani, IMEANDIKWA: Haki HUINUA Taifa.
Lazaro S Nyalandu, Mb.
Singida Kaskazini-CCM
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (TAIFA)
0 comments: