CCM MPYA NA TANZANIA MPYA AKINA LAZARO NYALANDU HAWATAKIWI.
Na Joseph Yona
Kwanza kabisa nianze kumshukuru kipenzi chetu Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Joseph John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazo zifanaya hasa kurudisha Tanzania yetu ambayo ilikuwa imepotea katika ramani ya haki na maendeleo.
Napenda niseme kwamba Dr Magufuli akili nyingi bana,na kwa moyo mkunjufu niseme tu hongera Rais wetu kwa uzalendo huo unaotuonyesha watanzania muda wote yeye anafikiri juu ya watanzania na Tanzania, na ndio maaana alikuwa halidhishwi na uongozi wa wizara ya utalii zamani wa Prof Jumanne Magembe, aliamua kumuondoa na kumuweka mchapakazi Dr Hamis Kigwangala
Dr Kigwangala katika wizara hii ni kama shamba la bibi,kaamaua kwa muda mchache kupiga kazi na leo tarehe 30 october 2017 kimetokea kile kilicho kuwa kimetarajiwa kwani aliye kuwa waziri wa wizara hiyo mzee wa matumizi na starehe Razalo Nyalandu ameondoka CCM
Kwangu mimi kuondoka kwa Razalo Nyalandu nilitegemea,siku itokee kwa kuwa anayo makando kando mengi ambayo tukiamua kuyasema anatakiwa akamatwe na afungwe maisha.
Leo tunapigania ccm mpya na Tanzania Mpya, nchi na chama cha Rais na mwenyekiti aliye na halufu nzuri katika uongozi na uzalendo wa kweli,watu kama Razalo Nyalandu watupishe walejee kwenye chama chao cha mafisadi kama CHADEMA.
Nani asiyejua kuwa Kuna kipindi Mbunge wa arumeru Joshua Nasari aliwahi kuongea kwa uchungu sana Namnukuu :-
Mh. Spika dalili za serikali iliyochoka ni Kama ya kuwa na Mawaziri Kama Razalo Nyalandu.
Anaendelea Yaani waziri wa maliasili kazi yake ni:-
Kupiga Picha na Mbwa wa wazungu,kupiga Picha ameshika risasi,kupiga Picha na helcopiter,kwenda na mamiss Kama Kina Anti Ezekiel nje ya nchi,tena kazi yake kubwa ni Kupiga Picha amebeba askari wa kike wa wanyamapori akiwa amemshika makalio na kumshika bega.
Mwisho Nassari aliomba uwaziri wa mambo ya ndani kumfundisha na kuwafundisha adabu sasa leo amepatikana Rais makini anayetaka maliasili zetu ziwanufaishe Watanzania wote hakika Razalo Nyalandu hafai kubaki CCM MPYA
Pia Nyalandu atambua kuna kipindi mbunge wa iringa mjini waziri kivuli wa maliasili aliwahi kumtuhumu kuwa ameuza nyala za serikali na kuruhusu zisafirishwe nchi za nje na biashara ya meno ya tembo ilishamili nchini chini ya uongozi wake Nyalandu.
Na hata biashara za ujangili pamoja na biashara haramu ndani ya mbuga zetu za Taifa zilisikika kila kona ya dunia na yeye akiwa kama kiongozi mwenye dhamana waziri wa wizara ya Maliasili na Utalii.
Leo Nyalandu bila hata kumuogopa Mungu anatamka CCM hii imepoteza uwelekeo,ila kipindi kile anakula bata kwenye shangingi la Waziri huku akitafuna chops za ngiri wa mikumi na ma miss wetu aliona ccm inafaa na iko katika uelekeo sahihi.
Wakati anashutumiwa kutafuna billion mbili za maliasili hapo ccm ilikuwa sawa chaaa!!!!
Wakati waziri huyo kivuli anakushutumu akionyesha video inayobainisha namna baadhi ya kampuni za uwindaji nchini zinavyo tumia vibaya leseni zao hapo ccm ilikuwa sawa aisee!!
Pia haya yote yanatokea kuna jangili kadakwa huko mbugani akiwa na risasi mia tatu hamsini na nane (358),nasikia amebanwa ataje mabosi zake na hii inanifanya nirudishe kumbukumbu kwenye Vita takatifu ya madawa ya kulevya aliyowahi piganiwa Paul Makonda,sasa Dr Kigwangala ameingia katika vita takatifu nyingine watanzania tumuunge mkono kwa kutoa ushirikiano.
Lakini vile vile nyalandu asitufanye tulio lala tukaamka,Nyalandu nakumbuka mkataba mbovu alioingia na wamarekani katika Mbuga yetu muhimu ya Selous wa kuchimba madini ya urenium,na anajua rais alivyo mkali kwenye Madini.
Nyalandu hajui kuwa alikuwa anataka kuwamilikisha wamarekani umiliki wa loliondo wa miaka mingi zaidi sema usalama wa taifa walikataa na akashindwa jaribio hilo.
Nyalandu hajui kuwa tunajua kuwa alimruhusu mkewe Faraja Kota kuuza vitaru vya wanyama poli kiholela ndani ya mbuga ya selous.
Nyalandu hajui kama tunajua maisha yake ya uwaziri alikuwa akanyagi ofisini au wizarani,ila kazi za wizara alikuwa akizifanyia hotelini southern sun.Yaani hajui tulikuwa tunapishana na mafaili ya wizara korido ya southern sun na kutumia gharama nyingi za wizara kufanyia kazi za wizara hapo hotelini kula kunywa na nk.
Au Nyalandu hajui kuwa tunajua alitumia mabilioni kwa mabilioni eti kutangaza mlima kilimanjaro ndani ya uwanja wa sunderland kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Au hajui kuwa mgogoro mkubwa na bodi ya utalii TTB walikwazana nae mwanzo,kabla hajawakamata kwa hongo bodi ilimshauri aangalie taratibu za manunuzi vizuri zisikiukwe akakataa na akaiingiza wizara hasarani naamini mpaka Leo wanalipa.
Pia hajui kuwa tunajua aliye kuwa mwiba mgumu kwake ni aliye kuwa mkurugenzi wa TTB Dr.Nzuki aliye mlazimisha akakataa,akawakamata wajumbe wa bodi hiyo akawashawishi wa muondoe Dr Nzuki kwa vyombo vya habari.
Au haju alivyo muondoa Dr.Nzuki akampeleka chuo cha utaliii na Dr Nzuki akaondoka kwenda Dubai.
Au Nyalandu hajui kuwa sisi masikini tuna mfuatilia sana Rais wetu mpendwa Dr Magufuli kuwa baada ya kuingia tu madarakani alichukua uwamuzi wa kumrudisha Dr.Nzuki na kumpa nafasi ya kuwa Naibu katibu Mkuu wa wizara ya maliasili na utalii.
Mwisho wenzangu na sisi ambao tunaona muelekeo mpya kabisa wa uzalendo anao chukua Rais wetu Dr Magufuli tunaendelea kumuunga mkono Rais kwamba yuko njia sahihi. Dr kigwangala upo njia sahihi songa fumua na weka mambo sawa ili watanzania wafaidi.
mwandishi ni
Mwenyekiti wa ccm tawi la bokorani na managing director wa pavea blog.
JOSEPH YONA.
0713 802 226.
0622 222 787.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: