Spika wa Bunge, Job Ndugai amemshukuru aliyekuwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah kwa utumishi uliotukuka.
Ametoa
shukrani hizo leo Jumatatu Ikulu jijini hapa baada ya Rais John
Magufuli kuwaapisha mawaziri, manaibu na Katibu wa Bunge mpya, Stephen
Kagaigai.
Spika Ndugai pia amewakaribisha mawaziri, manaibu na katibu huyo bungeni mjini Dodoma.
“Ninyi
mnatokana miongoni mwetu katika nyumba ile ya wabunge. Rais ameona
awape nyadhifa hizi, kubwa na la kipekee nimkaribishe Katibu wa Bunge
mpya Kagaigai na kipekee nimshukuru Dk Kashililah, asante sana kwa
utumishi uliotukuka hatutakusahau,” amesema.
Amesema
timu ya Baraza la Mawaziri ana imani nayo kwamba itafanya kazi vyema.
Baada ya kuapishwa leo, watakutana katika kikao cha Baraza la Mawaziri.
“Mje
Dodoma mmejiandaa, hii miaka miwili ya mwanzo walikuwa wanajifunza
funza, sasa tukienda Dodoma itakuwa ni kazi tu,” amesema Spika Ndugai.
Wakati
huohuo, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema kile walichokitamka
katika kiapo cha uadilifu wanapaswa kukizingatia kwa kufuata utaratibu
wa kisheria na Katiba ili kuepusha migongano.
0 comments: