Waziri,
George Mkuchika amefunguka na kuweka wazi mipango yake katika kutumikia
nafasi yake na kusema yeye ataanza kuhakikisha watumishi wa Umma
wanatumia muda wao kufanya kazi na hataki kusikia watumishi wameondoka
makazini kwenda kunywa chai.
Waziri
Mkuchika ambaye leo Oktoba 9, 2017 ameapishwa na Rais Magufuli kuwa
Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
amesema kuwa katika kipindi chake atahakikisha wafanyakazi wanalipwa
mshahara kulingana na kazi zao kweli, na wanatumia muda wa kazi kufanya
kazi za serikali.
“Kwanza
katika kipindi changu nikiwa Waziri kwa watumishi wa Umma, nataka
wananchi wanapofika maofisini wawakute maofisini, mara nyingi wengi
wanaripoti ofisini baada ya muda wanaondoka wanasema wanaenda kunywa
chai, yaani wananchi wanatoka vijijini wanamsuburi mtumishi aje eti
ameenda kunywa chai jambo hili kuanzia leo nitasimamia kuhakikisha
watumishi wa umma wanashinda kazini kwao ili kila mtumishi wa Umma
alipwe mshahara kwa kufanya kazi muda wote” amesema Mkuchika.
Aidha
Mkuchika amesema kuwa kwa sasa watumishi wengi wa Umma wanalipwa
mshahara kamili kwa kufanya kazi robo za serikali jambo ambalo yeye
atakwenda kulisimamia na kuhakikisha kuwa watumishi hao wanafanya kazi
kamili ili walipwe kulingana na kazi zao kamili.
Mbali
na hilo Mkuchika amedai kuwa atakwenda kuongea na Waziri wa Elimu ili
ikiwezekana somo la Rushwa lianze kufundishwa kuanzia shule ya awali
nchini mpaka vyuo vikuu na kusema watu wamekuwa wakichukua na kutoa
rushwa kwa kuwa hawana elimu ya kutosha juu ya athari ya rushwa.
0 comments: