Huyu Ndiye Miss Tanzania Aliyezua Gumzo Kubwa 1995!
Kushinda lile la Sitti Mtemvu mwaka juzi! ( Kutoka Maktaba ya Mwenyekiti, Majid Mjengwa.
Ilikuwa Septemba 3, 1995, Daily News
liliripoti, kuwa msichana wa miaka 18, Emily Adolph, pichani, Mwanafunzi
wa Central Secondary School, Dodoma, ndiye Miss Tanzania.
Hakukuwa na social media wakati huo,
lakini mjadala wa kwenye jamii ulioibuka. Ule wa Sitti Mtemvu mwaka juzi
hauwezi kuufikia. Tuliokuwepo tutakumbuka, kuwa tuliuona ni mjadala wa
ajabu kuwahi kutokea, maana mambo ya U-Miss nayo yalikuwa mapya kwetu.
Ikafika mahali mpaka Serikali ikaingilia kati kwa kumtafutia shule Emily baada ya kufukuzwa shuleni kwake..!
Tatizo lilikuwa umri wake, kuwa ulikuwa ni mdogo, wakati Sitti Mtevu tatizo lilikuwa hilo hilo la umri, alituhumiwa kufoji umri!
Sijui Emily Adolph yuko wapi sasa?
Kwa msaada wa Maggid Mjengwa,
Iringa.
Kwa msaada wa Maggid Mjengwa,
Iringa.
0 comments: