“Mimi na Dr. Slaa hatukusaliti vyama vyetu, tulisimamia misingi yetu” – Prof. Lipumba
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa wasaliti ni waliomleta Lowassa ndani ya UKAWA na sio yeye na aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Dr. Slaa kwa sababu walikuwa walisimamia misingi ya vyama vyao kama inavyosemwa.
Akizungumza kupitia Clouds 360 ya Clouds TV May 4, 2017, Prof. Lipumba amesisitiza kuwa aliwahi kumwambia Dr. Slaa kuwa anataka kugombea urais kupitia UKAWA, lakini naye Dr. Slaa alikuwa na nia hiyo.
“Mimi na Dr. Slaa hatukusaliti vyama vyetu, tulisimamia misingi yetu halisi ya vyama. Waliotusaliti ni wale waliomleta Edward Lowassa ndani ya UKAWA. Siyo sisi ambao tulijitoa ndani ya vyama vyetu.
“Nilizungumza na Dr. Slaa kuwa nilikuwa nataka kugombea Urais kupitia UKAWA-CUF, Dr. Slaa pia alihitaji kugombea.” – Prof. Lipumba.
About author: PAVEA BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: