Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa ACT
Wazalendo Samsoni Mwigamba na wanachama wengine 10 wametangaza kujiunga
na chama cha CCM baada ya kujivua uanachama wa ACT Wazalendo leo.
Taarifa za Mwigamba kujiunga na CCM
zimetolewa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kusema
kwamba wameamua kufanya hivyo ili kujitenga na upinzani unaokerwa na
maendeleo ya nchi, na pia kuunga mkono juhudi za serikali za mapambano
dhidi ya rushwa.
“CCM ya sasa ndicho chama
kinachotekeleza kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo
ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kukiasisi, nchi yetu ndio kinara wa
mapambano dhidi ya rushwa sasa hivi, sera ambazo ndio misingi ya ACT
Wazalendo, tumeamua kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya nchi
ili tuendelee kuwa sehemu ya mapambano katika kurejesha nchi kwenye
misingi yake”, amesema Mwigamba.
Samson Mwigamba atakuwa kiongozi wa pili
ACT Wazalendo kujivua uanachama wa ACT Wazalendo kwa mwaka huu baada ya
Prof. Kitila Mkumbo ambaye naye alifanya hivyo wiki kadhaa zilizopita.
0 comments: