Ni
kesi ambayo ipo Mahakamani Kisutu Dar es salaam kuhusu yule Mkazi wa
Chato mkoani Geita aliyetuhumiwa kwa kuandika habari za uongo Facebook
kuhusu kampuni ya Acacia na Serikali.
Mahakama ya
hakimu mkazi Kisutu imeipiga kalenda kesi hiyo inayomkabili Mkazi huyo
wa Geita Obadia Kiko mwenye umri wa miaka 41 hadi November 14, 2017 kwa
sababu upelelezi haujakamilika.
Mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la
kuchapisha taarifa ya uongo kupitia mfumo wa kompyuta na kuweka kwenye
mtandao wa Facebook, kinyume na sheria ya makosa ya Mtandao Namba 14 ya
mwaka 2015.Inadaiwa kuwa August 3, 2017 akiwa maeneo ya Chato Geita aliandika kwenye Facebook taarifa ifuatayo >>> “Taarifa kutoka kikao cha mazungumzo kati ya Serikali na Wawakilishi wa Kampuni ya Acacia kuwa Wanasheria wetu wanashindwa kutafsiri vifungu vya sheria hadi kufikia kuomba msaada kwa Wanasheria wa Acacia, sasa hivi ni vituko mwizi anakusaida sheria hahahaaaa”
Mazungumzo bado yanaendelea lakini Wanasheria wetu wanabanwa sana ukizingatia wale jamaa wana vielelezo vyote vya mikataba, kiukweli tumuombe Mungu maana Serikali ikitaka kuvunja mkataba na Acácia gharama kubwa zitatuhusu.
Lakini pia kuendeleza uvyama utatugharimu sana baada ya Mh.Rais Magufuli angewashirikisha wakina Mawakili wasomi waliokuwa wakali Tundu Lissu, Kibatala na Fatuma Karume kwenye mambo muhimu kama haya yeye kaleta Uchama sasa itatugharimu.
0 comments: