Aliyekuwa
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo baada ya kuteuliwa na kuapishwa
kuwa Waziri wa wizara hiyo amewaahidi Watanzania kuwa wategemee utendaji
mzuri wa kazi kutoka kwake huku akiwaomba watumishi wote umma kufanya
kazi kwa spidi.
Wakizungumza
Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kuapishwa, Mhe Jafo amesema
lengo lake ni kuisukuma nchi ifikie malengo yanayotarajiwa huku Dkt
Kigwangalla akisema Mh. Rais ameonyesha imani kubwa sana na uwezo wake.
“Kikubwa
zaidi niwaahidi Watanzani wategemee utendaji mzuri wa kazi, lakini
niombe sana watumishi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima
wajipange kufanya kazi kwa bidii , Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya,
Wakurugenzi naomba waongeze spidi na Wakurugenzi waongeze spidi lakini
watumishi wote waongeze spidi lengo ni tuisukume nchi yetu ifike katika
malengo tunayoyatarijia
Hata
hivyo Mhe. Jafo alipoulizwa kuwa ikiwa ni miongoni mwa Waziri
walipandishwa yeye anafikiri ni kwanini kapandishwa na kuwa Waziri
kamili? Akajibu “Ni mipango ya mwenyezi Mungu jambo la kwanza, la pili
ni imani ya Mheshimiwa Rais kwangu, tatu ni utendaji wa kazi kwasababu
ni lazima popote utakapo niweka ni lazima nifanye kazi kwasababu nina
dhamana ya Watanzania naamini popote Mungu ananiona.”
Kwa
upande wake aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya ambaye kwasasa ni Waziri wa
Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla amesema kuwa “nimefarijika sana
pia nimepewa imani kubwa na Mhe. Rais, nimepewa Wizara nyeti ni wizara
ambayo inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa ni wizara nyeti sana,
na mimi kupewa jukumu hili maana yake mhe. Rais ameonyesha imani kubwa
sana na uwezo wangu lakini pia na uzalendo nilionao naomba niwaambie
Watanzania na Mhe. Rais Kuwa sitawaangusha.”
0 comments: