ACT katika taarifa yake jana Jumapili,
imesema Rais ameamua kuyaweka pembeni matakwa ya sheria yanayoongoza
mchakato wa uteuzi wa Katibu wa Bunge na kuamua kujichagulia apendavyo.
“Kutokana na unyeti wa nafasi ya Katibu
wa Bunge, na kwa minajili ya kuweka 'check and balance' pamoja na
kulinda uhuru wa Bunge, kwenye mchakato wa uteuzi wa nafasi husika,
sheria imeweka utaratibu wa kufuatwa kwenye uteuzi wa Katibu wa Bunge,”
imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Ado Shaibu ambaye ni katibu wa
itikadi, mawasiliano na uenezi wa ACT Wazalendo.
Amesema mbali na Rais kuwa na mamlaka ya
kumteua Katibu wa Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 87 ya Katiba ya Jamhuri
ya Muungano, anapaswa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Sheria ya
Utawala wa Bunge ya mwaka 2015.
Kwa mujibu wa kifungu cha 7(3) cha
sheria hiyo, Rais atateua jina moja kutoka miongoni mwa majina matatu
yaliyopendekezwa na Tume ya Huduma za Bunge.
Shaibu amesema jambo hilo si la hiari bali ni sharti la lazima la sheria ambalo Rais analazimika kulifuata.
Ndiyo maana kifungu husika kinasema, “The Commision shall recommend three names. (Tume ni lazima ipendekeze majina matatu)”.
ACT imesema wajumbe wa Tume ya Huduma za
Bunge kwa taarifa ambazo chama hicho kinazo, hakuna kikao chochote
kilichoketi na kupendekeza majina kwa Rais kwa ajili ya uteuzi wa Katibu
wa Bunge.
Chama hicho kimesema uteuzi huo ni ushahidi wa wazi wa kudharauliwa mhimili wa Bunge.
“Ni matumaini yetu kuwa Bunge na watu
wote wanaopenda uhuru na uimara wa Bunge watasimama imara kuupinga
uteuzi huu ambao ni kinyume cha sheria,” amesema.
ACT imesema iwapo Rais hatatengua uteuzi
huo na kufuata utaratibu uliowekwa na sheria za nchi, kitalifikisha
suala hilo mahakamani ili kupata ufafanuzi wa Mahakama.
“Ni wakati muafaka kwa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuishauri Serikali kwenye
masuala ya kisheria kuwajibika,” imesema taarifa hiyo.
0 comments: