Mhandisi Emanuel Manlabona akimuonyesha Naibu Waziri Nishati Subira
Mgalu Juu ya uwezo wa kituo hicho cha kusambaza umeme kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Usafirishaji Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa
Mhandisi Emanuel Manlabona akimuonyesha Naibu Waziri Nishati Subira
Mgalu Juu ya uwezo wa kituo hicho cha kusambaza umemekulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Usafirishaji Umeme Mhandisi Bishaija Kahitwa
Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu kulia akisalimiana na mkazi wa Mbagala
****
Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu amewahakikishia wakazi wa
Mbagala umeme wa uhakika kwani wizara ya nishati kwa kushirikiana na
wataalamu mbalimbali wa TANESCO wanafanya jitihada za kutosha
kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana ili kuwezesha matumizi ya
viwanda mbalimbali vilivyopo mbagala na matumizi
ya Nyumbani kwa wakazi wa Mbagala.
“Tumesikia matatizo yenu yanayohusiana na Umeme,
ila Napenda kuwahakikishiani kuwa Wizaraya Nishati pamoja na TANESCO
kwa ujumla tunafanya kazi, kuhakikisha umeme mbagala unakua wa
Uhakikia, leo hapa nimekuja kutembelea hiki kituo cha usambazaji
umeme cha mbagala , ambacho kinajengwa na kwa kushirikiana kwa pamoja,
tunapambana kituo hichi kikamilike ndani yam waka huu mpaka kufikia
Disemba , kituo hiki kiwe kimekamilika".
Hayo aliyazungumza jana katika ziara aliyoifanya
katika vituo vya kusafirisha umeme, kituo cha Mbagala na Kurasini
lengo kubwa ikiwa ni kuangalia hali halisi ya utendaji wa TANESCO
katika
kuhakikisha wananchi wanapata huduma hii ya Nishati ya umeme wa uhakika.
0 comments: