Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya mazungumzo na Taasisi
muhimu za kifedha na kiuchumi nchini China kwa ajili ya upatikanaji wa
fedha za uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na viwanda nchini .
Ujumbe
wa TADB umeoongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki , Francis
Assenga alipokutana na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo
ya China (CBD) leo kwenye Mkutano uliofanyika, Guangzhou, China.
Pande
zote mbili zimekubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano
utakaowezesha kupatikana kwa fedha kwenye uwekezaji wa miundo mbinu ya
kilimo na viwanda vidogo vidogo vya uongezaji thamani kwenye mazao ya
kilimo kwa wakulima nchini.
Katika
ziara hiyo TADB pia imefanya majadiliano ya kina na Mfuko wa Maendeleo
ya Africa wa China (China African Development Fund) ambao hufanya
uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na ya kibiashara (Equity
investmenta) kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Mazungumzo
hayo yamehudhuriwa na Ujumbe wa ulioongozwa na Makamu Mtendaji wa Rais
na Naibu Mtendaji Mkuu wa 'CADFUND' . Wang Yong aliyefuatana na
Mkurugenzi Mkuu wa Sekta ya Viwanda, Kilimo, Afya na Uwekezaji, . Lei
Ma; Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Masoko na Huduma Elekezi , Henry Liu
na Meneja wa Uwekezaji wa Viwanda, Ardhi na Kilimo Luo Zhongquan.
Ujumbe
wa Tanzania umeongozwa na Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji
(UWEKEZAJI), Prof. Adolf Mkenda. Wengine waliohudhuria ni Balozi wa
Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki; na Afisa Ubalozi wa Tanzania
nchini China Lusekelo Gwassa.
Katika
mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine CADFUND walikubali kuendelea
kutoa fedha kwenye miradi ya kiuchumi na uwekezaji mkubwa kwenye nyanja
za kilimo, madini na miundombinu kama ya maji na umwagiliaji.
0 comments: