
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo” wilaya ya Shinyanga
ambapo jumla ya wahitimu 238 wamefuzu mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda
wa miezi minne.
Sherehe za kufunga mafunzo hayo zimefanyika leo Jumatatu Oktoba 9,2017 katika viwanja vya Sabasaba mjini Shinyanga.
Akizungumza katika sherehe hizo,Mkuu
huyo wa wilaya aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kutumia vyema mafunzo
waliyoyapata huku akiwaasa kufanya shughuli za maendeleo ili kujiinua
kiuchumi.
Matiro aliwataka wahitimu hao kuunda vikundi vya ujasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia.
“Mmejifunza mambo mengi,naomba
muzingatie mlichojifunza,muwe wazalendo wa nchi yetu,kuweni mstari wa
mbele kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kuwafichua wahalifu
na wale wote wanaoleta uvunjifu wa amani katika jamii”,aliongeza Matiro.
Katika hatua nyingine alizitaka kampuni za ulinzi kutumia walinzi waliopitia mafunzo ya mgambo.
Naye Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya
Shinyanga Meja Ford Mwakasege alisema washiriki wa mafunzo hayo mwaka
huu wengi wametoka katika makampuni ya ulinzi.
“Mafunzo haya yameanza Juni 5,2017
washiriki wakiwa ni 303 lakini leo wamehitimu 238 kati yao wanaume ni
193,wanawake ni 45,na yalikuwa yanaendeshwa na wanajeshi na wanajeshi wa
kujitolea,wahitimu pia walishiriki zoezi la upandaji miti
lililozinduliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga hivi karibuni”,alieleza Mwakasege.
Aidha alisema miongoni mwa changamoto
zilizopo ni ukosefu wa sare za jeshi la akiba na utoro kwa washiriki
hali inayofanya wengi kutomaliza mafunzo.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa
mafunzo hayo,Chacha Warioba alisema miongoni mwa mambo waliyojifunza
kuwa ni pamoja na matumizi ya silaha mbalimbali,kwata,rushwa,usalama wa
taifa na zimamoto na uokoaji.
Hata hivyo alisema changamoto kubwa kwao
ni ukosefu wa ajira hivyo aliiomba serikali iwape kipaumbele katika
ajira zinazojitokeza.
Aliitaja changamoto zingine kuwa ni
ucheleweshaji wa vyeti vya mafunzo na malipo duni kwenye makampuni
wanakoajiriwa hivyo kuiomba serikali kutoa mwongozo wa kima cha chini
cha mishahara kwenye makampuni.
Mwandishi wetu,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakiwa wamebeba silaha zao
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua gwaride
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa mafunzo hayo wakisubiri kukaguliwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Meza kuwa wakiwa wamesimama wakati wahitimu wakipita kwa mwendo wa polepole
Wahitimu wa mafunzo hayo wakipita kwa mwendo wa taratibu/polepole mbele ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Wahitimu wa kike wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro
Wahitimu wakitembea kwa mwendo wa polepole
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita kwa mwendo wa haraka
Wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba wakipita kwa mwenda wa haraka mbele ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
Mkufunzi wa mafunzo ya Jeshi la Akiba na MC wakati wa sherehe hizo,Sajenti Geofrey Kamala akitoa maelekezo
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mhitimu Chacha Warioba akisoma risala
Wahitimu wa mafunzo hayo wakiimba wimbo
Wahitimu wakiimba shairi
Wahitimu wakionesha mchezo wa Singe
Burudani inaendelea
Wahitimu wakionesha mchezo wa ngumi

Wadau mbalimbali wakiwa eneo la tukio
Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege akitoa taarifa kuhusu mafunzo ya jeshi la akiba
Mshauri wa Mgambo wa wilaya ya Shinyanga Meja Ford Mwakasege akizungumza
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo”
wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga mafunzo mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo”.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba “Mgambo”
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na wakufunzi wa mafunzo hayo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine
Matiro akipanda mti katika shule ya msingi Uhuru iliyopo jirani na
uwanja wa Sabasaba palipofanyika sherehe za kufunga mafunzo ya jeshi la
akiba.
0 comments: