Mifupa iliyokutwa ni pamoja na taya yenye meno,mbavu,mfupa mmoja wa paja,mifupa mitatu ya mikono.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo
jioni Jumatatu Oktoba 9,2017 wakati wananchi wakichimba kisima ndani ya
bwawa hilo ambalo limekauka.
“Kutokana na tatizo la ukame,wananchi walikuwa wanachimba kisima kwenye
bwawa ambalo hivi sasa limekauka,wakati wanaendelea kuchimba ndiyo
wakaona mifupa ya binadamu,hatujajua huyo mtu alifariki kwa njia
gani,pengine alitumbukia kipindi bwawa lina maji ama alifukiwa na watu
wasiojulikana”,kilieleza chanzo cha habari cha Malunde1 blog.
"Mifupa iliyokutwa ni taya yenye meno,mbavu,mfupa mmoja wa paja,mifupa mitatu ya mikono",kimesema chanzo chetu cha habari.
Mkuu wa kituo cha polisi kituo cha Tinde pamoja na mbunge wa Viti Maalum
mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal (CCM) wamefika eneo la tukio.
Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde kupitia blog yako pendwa ya Malunde1 blog.
Mwakilishi wa Malunde1 blog – Tinde,Said Nassoro ametutumia picha kutoka eneo la tukio,Tazama hapa chini
Mifupa inayodaiwa kuwa ni ya binadamu iliyokutwa kwenye bwawa la Tinde
Mifupa hiyo
Shimo ambamo kumekutwa mifupa
Wananchi wakishangaa
Wananchi wakishangaa mifupa hiyo
Mwananchi akishangaa mifupa hiyo
Mwananchi akikusanya mifupa hiyo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal,mkuu wa kituo cha polisi Tinde na wananchi wakiwa eneo la tukio
Sehemu ya bwawa la Tinde likiwa limekauka
Bwawa likiwa limekauka
0 comments: