Rais
Yoweri Museveni amemvisha Mtukufu Prince Karim Aga Khan IV nishani ya
juu ya heshima barani Afrika (Most Excellent Order of Pearl of Africa,
The Grandmaster) ili kutambua miongo kadhaa ya mchango wake katika
maendeleo ya Uganda.
Museveni
alimvisha nishani hiyo Jumatatu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bushenyi-Ishaka katika wilaya ya
Bushenyi.
Mtukufu
Aga Khan, ambaye ni Imam wa madhehebu ya Ismailia, kupitia taasisi ya
Aga Khan ana miradi mingi ya maendeleo katika nyanja za elimu, nishati,
afya, hoteli na utalii, vyombo vya habari.
Aga
Khan aliwasili nchini Uganda Jumapili kuwahi maadhimisho ya miaka 55 ya
uhuru na alikuwa na kikao na Rais Museveni pamoja na maofisa waandamizi
wa serikali katika Ikulu ya Entebbe.
Mapema
wakati wa utoaji taarifa kwa waandishi wa habari katika Kituo cha
Habari Uganda, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Esther Mbayo
alidokeza sababu za kumtunukia nishani hiyo ya heshima Aga Khan.
“Atatunukiwa
nishani ya heshima ya juu kwa sababu ya mchango wake mkubwa wa kiuchumi
alioutoa kwa nchi yetu duniani kwa ujumla,” alisema Mbayo.
0 comments: