Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumanne Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa
Mlipakodi, Richard Kayombo amesema makusanyo hayo ni hatua nzuri
kuelekea lengo la mwaka ambalo ni Sh17 trilioni.
Ametoa mchanganuo wa makusanyo hayo kwa kila mwezi ambao umeonyesha kuwa wamekusanya zaidi ya Sh1 trilioni.
“Julai
tulikusanya Sh1.1 trilioni, Agosti Sh1.2 trilioni na Septemba Sh1.3
trilioni. Watu wamekuwa wakitaka makusanyo hayo yawe yanasomwa kila
mwezi lakini tukitoa kila robo ya mwaka tunaonyesha kiasi kwa kila
mwezi,” amesema Kayombo.
Ukizidisha
makusanyo hayo mara nne ambayo ni tafsiri ya mwaka mzima jumla inakuwa
Sh14.6 trilioni lakini Kayombo anasema makusanyo ya robo moja hayawezi
kutoa picha ya jumla kwasababu misimu ya biashara inatofautina hivyo ana
matumaini lengo litafikiwa.
Amevitaja
vyanzo vikuu vya mapatio kuwa ni viwanda, ajira na uingizaji wa bidhaa
lakini amesema vyanzo hivyo hutoa kodi zaidi kulingana na wakati.
Kadhalika
Kayombo amewakumbusha wamiliki wa majengo nchi kulipa kodi zao mapema
badala ya kusubiri mwishoni mwa mwaka na kusababisha misongamano na
usumbufu usio wa lazima.
Pia
wamewataka wenye michezo ya bahati nasibu wametakiwa kulipa kodi zao
kama sheria inavyoelekeza. “Anayepaswa kulipa kodi kwa wiki alipe na
anayepaswa kulipa kwa mwezi au mwaka naye afanye hivyo.”
Kayombo
amewataka wananchi kutumia na kuziamini takwimu zinazotolewa na mamlaka
hiyo kwani takwimu zote nyingine kuhusiana na mapato ambazo
hazijatolewa na TRA sio za kuaminika.
0 comments: