HAINGII AKILINI NA HAIINGII AKILINI HATA KIDOGO.
Na Joseph Yona
Taifa letu pedwa lenye amani Tanzania,Mungu aendelee kutusaidia na tunawashukuru viongozi wetu waliopita kuliongoza Taifa hili katika awamu zilizotangulia nne.
Sasa tuko kwenye awamu ya tano ya “hapa kazi tu”.
Katika awamu hii ya tano ya “hapa kazi tu” kwa kipindi kifupi, tumeshuhudia Rais Dr. Joseph Magufuli akifanya mambo ambayo watanzania wanamuunga mkono kila sehemu.
Leo hii nimeamua kuja na maada ya ilikuwa haiingii akilini hata kidogo, baada ya kutafakari mambo mengi ya hovyohovyo yaliyokuwa yanaendelea katika taifa hili.
Kitu ambacho nimegundua viongozi wetu wakuu waliopita au wastaafu,walikuwa wanawaamini sana wataalam na waliokuwa wamewateua.
Ilikuwa haiingii akilini hata kidogo, Twiga mrefu kachukuliwa kwa kuswagwa kutoka mbugani kama serengeti,ngorongoro , manyara na mikumi mpaka uwanja wa ndege, mamlaka hazioni.
Twiga huyo kafikishwa uwanjani, kaingizwa kama ni mzima mzima au kwa kupindishwa shingo kwa lazima au kwa hiyari,au kwa kusokota shingo mie simo, halafu mamlaka hazioni.
Mwisho twiga anasafirishwa mpaka uarabuni waandishi wakajua, wakaripoti mamlaka kimya halafu mamlaka hizo zilibaki, haiwezekani.
Ilikuwa haiingii akilini hata kidogo,eti kuna baadhi ya maeneo katika Taifa hili ukifika na simu yako inaandika kuwa karibu falme za kiarabu, haiwezekani.
Ilikuwa haiingii akilini hata kidogo, ofisi moja cheo kimoja mtanzania, mkenya na mwarabu au mhindi mmeajiriwa halafu mkenya, mwarabu na mhindi wanapewa mshahara mamilioni, wanapewa usafiri, wanapewa kodi ya nyumba,mawasiliano na marupurupu kibao ilhali mwajiriwa mtanzania anapewa laki tano bila nyumba wala usafiri halafu unasema watanzania wavivu”Hapana”.
Tena ajabu na kweli aingii akilini kwa mtanzania mwenye cheo kikubwa analipwa laki tano, wakati watu wa chini yake wakenya,warabu, wahindi wanayo mishahara na marupurupi makubwa, halafu mkurungezi anakwambia nyie watanzania wavivu.
Haiwezekani na ilikuwa haiingii akilini hata kidogo na haiingii,kwa mwenzako kutoka nje hana shida,hana mawazo ya kuwaza maji , umeme,kodi ,daladala za mbagara wala matibabu ya familia, ili hali mtanzania yeye jua lake, shida zake, tabu zake, matibabu yake, halafu muwe sawa atakudharau uwe bosi au kawaida.
Ilikuwa haiingii akilini hata kidogo, eti Tanzania inatumia mabilioni ya shilingi kwa ajili ya kusafiri viongozi kibao nje,ilahali wagonjwa muhimbili na hosptali nyingine hazina vitanda wala maabara.
Yaani mimi ilikuwa haiiniingii akilini hata kidogo, baadhi ya maofisi ya serikali, viongozi wakubwa na hata viongozi wa taasisi za afya wakifanya semina za fedha, vikao vya kulipana ,sherehe za kupongezana ilhali wagojwa na madawa hakuna, madirisha ya hospitali hayana nyavu za kuzuia mbu, haiwezekani.
Haiingii akilini na haiewezekani eti matatizo yote makubwa yanayozikuta taasisi muhimu zinatotoa huduma muhimu za kijamii, lakini vigogo wakinunua magari ya kifahari,wakienda kutibiwa nje, kutibu mbwa zao nje, kula starehe nje haiingii aisee.
Binafsi ilikuwa haiingii akilini hata dakika moja eti Tanzanite inachibwa Tanzania, inazalishwa Tanzania lakini Taifa hili katika wauzaji wakubwa duniani hawapo na ni moja ya Taifa ambalo si muuzaji mkuu wa Tanzanite duniani aah!.
Ilikuwa inatatiza sana na haiwezekani na haimo kwenye akili kuwa makontena kwa makontena ya mchanga wa madini yenye thamani kubwa ukipakiwa kwenye bandari zetu ukienda nchi za wenzetu kuchakatwa.Ilihali uwezo wa kuwekeza mitambo ya kuyachakata madini hayo tunao na tunawafanyabiashara wakubwa wenye mitaji tena wazawa.
Kwa kuwa ni maajabu sana , tena sana na haikubaliki na haiingii akilini, eti viwanda vyetu maeneo mengi ya nchi, hasa Morogoro vimegeuka kuwa magofu na mabanda ya kufuga wanyama ila hali wabunge wetu wakilipana posho za kufa mtu,sherehe za kila aina pesa hizo zingejenga au zingefugua viwanda vingapi?.
Yaani kwa leo haingii akilini hata kidogo eti TRA wameshindwa kuendelea kukaa na wafanyabiashara kuwaelimisha matumizi ya matumizi bora ya EFD machine,ila uwezo wa TRA ni kufunga biashara.
Yaani TRA watambue kuwa suluhisho la kufungia biashara kwa siku au miezi ni kuuendelea kupoteza mapato ya serikali,suluhisho ni kuendelea kuzungumza na wafanyabiashara kuwajengea uzalendo wa kuipenda nchi yao.
Ilikuwa hainingii akilini hata kidogo , usumbufu mkubwa wanaoupata wafanyabiashara wakubwa kwenye biashara zao. Nashukuru Mh. Rais alishawahi kusema serikali yake haitaruhusu urasimu wa vikodi kodi na vitaasisi vingi katika kuendesha biashara zao. Na nashukuru Rais aliwahi sisitiza wawe wazalendo na walipe kodi usumbufu atawaondolea. Mfano, wa hilo ni kwa mfano wamilikiwa vituo vya mafuta tu kuna taasisi kama nane au zaidi zinazokata kodi na vikorobwezo vingi tu.Katika vituo vya mafuta kuna EWURA,TRA,WMA,OSHA,TBS,FIRE, huko juu kuna I.T.S,SBS nk.
Hapa nieleweke ukweli ni kuwa tatizo sio kodi,ila majukumu yao mengi yanaingiliana tu mfano TBS au EWURA tu zingeweza kufanya kazi za OSHA , I.T.S, S.B.S nk.
Ilikuwa haiingii akilini , eti mtu mmoja ni mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa na wakati huohuo ni mbunge wa kuchaguliwa au kuteuliwa na wakati pia ni mjumbe wa bodi wa shirika fulani haipo akilini,kwa kuwa mtu huyo kwenye vikao vya bunge na semina zenye posho nono, tamu hawezi kuziacha eti afanye kazi za mkuu wa wilaya au mkoa.
Kwa hiyo ukikaa ukatafakari ndio unaelewa umuhimu wa kumpata Deng Xiao Ping wa Tanzania , Rais Joseph Magufuri.
Ilikuwa hainiingii akilini kabisa , eti barabarani za enzi za baba wa Taifa, mfano barabara ya njia ya Tanga zipo mpaka leo nzima na imara kabisa.
Lakini barabara nyingi nchi hii ukarabati kila mara,mfano barabara ya kilwa,temeke mwisho,zinaidhinishwa pesa nyingi za ukarabati ili hali hospitali ya Temeke na nyingine nyingi ni aibu kuziona.
Ilikuwa ni ngumu kumeza na hainiingii akili nikiwa nafanya kazi chuo kikuu, Maprofesa na madaktari,wakiisema serikali kuhusu posho za semina na vikao.Ilihali wao kila siku semina,vikao,posho,utafiti wa uongo na kweli,kuidhinisha mamilioni ya kununua madawa ya maabara, viyoyozi,samani nk wakati huo vyoo vya wanafunzi vibovu vichafu, mabweni aibu tupu.
Ilikuwa hainingii akilini kabisa, eti mkuu wa wilaya na mkoa wakiitisha mkutano wa wananchi,ili kuzungumzia kero zao,wakija na msafara wa magari zaidi ya kumi,kuja kuzungumza na maskini wasio na msosi, madawa, karo nk.
Ilikuwa haiji wala hainiingii akilini kabisaa, kijana mdogo msomi au sio msomi anaajiriwa bandarini.,T.B.S,T.R.A na,T.F.D.A nk baada ya wiki mbili anamiliki prado,kiwanja na anajenga gorofa baada ya miezi minne, duu haikubaliki.
Ilikuwa haiji wala hainiingii,eti diwani ambaye hana mshahara anazo posho tu akimaliza kipindi chake cha miaka mitano ana mahoteli, majumba nk ili hali wananchi wake aliwaahidi kwa unyenyekevu wakiwa kwenye lindi la umaskini afya mbovu huduma za msingi mbovu, haikubaliki
Bado sana haitaniingia akilini, eti baadhi ya viongozi wetu wabunge mawaziri, wapinzani wakijiita wazalendo wa taifa hili wakati wao wakimiliki vitega uchumi vikubwa, mahotel,majumba, mapesa nje ya nchi na ndani na magari ya kifahari sana wakati hospital zetu ni mbovu, wananchi sisi ni fukara.
Tena ajabu na kweli imetokea kwa anayejiita mzalendo mkiti wa chadema taifa jimboni mwake HAI,katika hospitali ya machame kukosekana vitanda vya wagonjwa ilhali anao mshahara,marupurupu na pesa za mfuko wa jimbo.
Tena ajabu na kweli ni kuwa mtanzania huyu anayejiita mzalendo alikuwa akikalia jengo la NHC kwa miaka mingi akifanya biashara haramu bila kulipa kodi wala mapato ya serikali.
Bado sana hainiingii akilini kabisa eti maji ya matumizi ya Dar es salaam yanatokea mto Ruvu, halafu masaki maji yanamwagilia maua,nyasi masaa 24, wakati wakazi wa kibaha , chalinze,mlandizi,bagamoyo nk hawana maji ni shida tupu haikubaliki.
Wakati natafakari haya yote nashukuru tumempata jembe letu, Dr. Joseph Magufuli ambaye kwa moyo mweupe kutoka moyoni anazijua shida zetu watanzania. Rais ukweli haijawahi tokea ghafla kiongozi akawa maarufu na anasemwa vizuri sana,hakika utaandikwa na wino wa dhahabu.
NI MKITI WA TAWI LA BOKORANI
Ni Joseph Yona (0713 802226
About author: PAVEA BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: