Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Simon Haule
amethibitisha kuokotwa kwa viungo vya mwili wa binadamu katika bwawa la
maji la Jomu wakati watu wakitafuta maji huko Tinde mkoani Shinyanga.
Akiongea
na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Kamishna
Msaidizi Simon Haule alidai kuwa iku ya Jumatatu watu walipoona viungo
hivyo vya binadamu ilibidi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi na wao
walifika na kukuta viungo hivyo.
"Fuvu la kichwa limepatikana hapo bwawani, taya ya binadamu, mbavu za binadamu kumi na nne.
"Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo jeshi la polisi lilichukua hatua za haraka kufika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa awali tukishirikiana na daktari mtaalam wa viungo vya binadamu
"Katika tukio hilo tulikuta viungo hivyo ikiwa pamoja na mfupa mmoja wa sehemu ya paja, mifupa ya mikono na mifupa ya sehemu ya bega ya binadamu" alisema Simon Haule

0 comments: