Rais
Uhuru Kenyatta amemjia juu Kiongozi wa NASA Raila Odinga baada ya
kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika
Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya na kusema hata kama amejitoa Katiba ya
Kenya haijazuia uchaguzi kutofanyika
Kenyatta
amesema kuwa Odinga alitaka uchaguzi urudiwe jambo ambalo limeigharimu
nchi ya Kenya fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara,
zingeweza kutumika kujenga mahospitali na kutoa huduma mbalimbali kwa
wananchi, lakini anashangaa mtu ambaye ametaka uchaguzi kurudiwa
anajiengua tena.
"Rafiki
yangu nasikia sasa umesema umejitoa baada ya kutupeleka peleka zaidi ya
shilingi bilioni 12 hivi sasa zinatumika ili tufanye uchaguzi, pesa
ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingetumika kujenga
hospitali ya wananchi sasa zinatumika kwa uchaguzi ambao yeye ndiye
aliitisha na sasa anasema hataki, kuna haki hapa jamanii, si mahakama
ilisema IEBC haina makosa hayo masharti yote unatoa lakini tume hii si
ndiyo imefanya viongozi hawa wengine wote kupatikana" alihoji Kenyatta
Mbali
na hilo Kenyatta amesema kuwa wao wataendelea na mchakato wa uchaguzi
kama kawaida na kusema huenda awepo au asiwepo Odinga uchaguzi
utafanyika kama kawaida kama ambavyo tume ya uchaguzi ilitangaza.
0 comments: