
Kesi
inayomkabili Mbunge wa Geita na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi
Mkoani Geita Joseph Kasheku Msukuma na madiwani nane imesogezwa mbele
baada ya upande wa mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.
Kesi
hiyo ambayo ilikuwa isikilizwe jana imepangwa kutajwa tarehe 10 mwezi
wa 11 mwaka huu ambapo washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana.
Kwa
upande wake wakili anayewatetea washitakiwa Bw Deo Mgengeli alielezea
hatua ambayo imeendelea siku ya jana mahakamani hapo kuwa shauri
limekuja na kwamba limetajwa na hadi sasa hakuna mshitakiwa ambaye
ameongezeka hivyo mahakama imeamua tarehe Kumi mwezi wa 11 wawasili
mahakamani kusikiliza tena kesi hiyo.
Aidha
wakili Mgengeli alizungumzia suala la madiwani wengine waliokamatwa na
jeshi la polisi na kutofikishwa mahakamani akasema kuwa kukamatwa kwa
madiwani hao ni jambo la kawaida kwani ni swala la upepelezi kwa
makosa ya jinai na kwamba alhamisi wanatakiwa kwenda tena polisi ili
kujua ni kipi ambacho kinaendelea ila hadi sasa hawana kosa lolote.
Awali washitakiwa hao kwa pamoja walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Geita Septemba 19 mwaka huu
Washitakiwa
wanakabiliwa na mashitaka ya kufanya mkutano bila kibali, kuziba
barabara na uharibifu wa bomba la maji linaloelekea kwenye mgodi wa
dhahabu wa GGM.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
0 comments: