Kairuki
ameyasema hayo jana tarehe 10 Oktoba, 2017 jijini Dar es Salaam
alipozungumza na watumishi wa Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake,
waliopo Dar es Salaam na Makao Makuu ya Wizara Dodoma.
Lengo
La kikao hicho lilikuwa ni kufahamiana na kupanga mikakati ya
kushirikiana ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango
mkubwa katika ukuaji wa Uchumi wa nchi.
Taasisi
zilizoshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Chuo cha Madini
Dodoma (MRI) pamoja na Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini
na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji
(TEITI).
Alisema
kuwa Sekta ya Madini inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa wa ukuaji wa
uchumi wa nchi na kuwataka wataalam wa madini kubuni mbinu za ukusanyaji
wa maduhuli pamoja na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwenye uchimbaji
madini.
Katika
hatua nyingine aliwataka wataalam hao kubuni mikakati ya kuzuia
utoroshaji wa madini nchini ili nchi ipate mapato stahiki.
Aliwataka
watumishi kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwa wabunifu ili sekta
hiyo iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Naye
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo aliwakumbusha watumishi
kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara ikiwemo kufanya kazi kwa tija ili
hatimaye sekta ya madini iweze kuchangia katika uchumi wa nchi kwa kuwa
mchango wa sekta husika bado ni kidogo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
0 comments: