Bwana Odinga anasema anataka kufanyika uchaguzi mpya jinsi ilivyoamuliwa na mahakama ya juu.
Uchaguzi
huo wa tarehe 26 utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama
ya juu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti
mwaka huu.
Bw.
Odinga anasema amejiondoa ili kuipa tume ya uchaguzi IEBC muda wa
kutosha kufanya mabadiliko ambayo yatawezesha kufanyika uchaguzi kwa
njia nzuri.
Awali
tume ya uchaguzi ilikuwa imemtangaza rais wa sasa Uhuru Kenyatta kuwa
mshindi.Ilisema kuwa Bw. Kenyatta alishinda uchaguzi huo kwa kura
milioni 1.4.
Upinzani
nchini Kenya awali ulikuwa umetangaza wazi kuwa ungeshiriki kwenye
uchaguzi mkuu ikiwa mabadiliko yanayostahili yangefanyika.
Upinzani
unaamini kuwa uchaguzi unastahili kufutwa baada ya Odinga kujiondoa, na
kutoa muda wa kutosha kufanyika mabadiliko yanayostahili ili uchaguzi
kufanyika kuambatana na sheria na katiba.
Serikali
imekuwa ikisema kuwa uchaguzi utafanyika na rais kuapishwa.Bw. Odinga
pia ametoa wito kwa watu kuandamana Jumatano hii kwa kutumia kauli mbiu
"hakuna mabadiliko, hakuna uchaguzi".
Mwezi
Septemba mwendesha mashtaka mkuu nchini Kenya Keriako Tobiko,
aliamrisha polisi na tume ya kupambana na ufisadi kuchunguza ikiwa
wanachama wa tume ya uchaguzi walihusika na uhalifu wowote.
Alitaka wachunguzi kuchunguza madai kuwa maafisa wawili wakuu wa upinzani walikuwa wamedukua mitandao ya tume ya uchaguzi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
0 comments: