Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
imesema idadi ya watu waliofariki dunia kwa kunywa kinywaji
kinachosadikiwa kuwa gongo imefikia 10.
Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa
amesema leo Alhamis kuwa wananchi walitoa taarifa baada ya hali za
waliotumia pombe hiyo eneo la Kimara kubadilika.
Amewataja waliofariki dunia kuwa ni
Mohamed Issa (67), Kabugi Rashid (64), Stanslaus Joseph (58), Stephen
Isaya (61), Monika Rugaillukamu (42), Alex Madega (41), Hamis Mbala (35)
na Ekson Nyoni (28).
Wengine ni mwanamke aliyekuwa akiuza
pombe hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Anoza na Maleo Ramadhan (45)
mkazi wa Kimara Stop Over.
Kamanda Mambosasa amesema katika
upelelezi wa awali wamebaini chupa tatu za ujazo wa lita moja zikiwa
zimejazwa pombe inayodhaniwa kuwa ni gongo.
"Vielelezo vyote vya tukio hili vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo," amesema.
Amesema upelelezi unaendelea kubaini
wote waliohusika katika tukio hilo, akiwataka wananchi kuacha kunywa na
kula vitu visivyo na ubora wala kuhakikiwa na mamlaka husika.
0 comments: