Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi ameshiriki
zoezi la uvunjaji wa nyumba kwa kuvunja nyumba yake kwa hiari iliyokuwa
imejengwa ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi wa barabara.
Waziri
Lukuvi amevunja nyumba yake iliyokuwa imejengwa katika eneo la hifadhi
ya barabara kuu iendayo katika hifadhi ya Ruaha katika Kijiji cha
Mapogolo, mkoani Iringa.
“Kama
kiongozi nimeamua kuonyesha mfano kumuunga mkono Mhe. Magufuli ambaye
ameamua kuiboresha barabara hii kuwa kiwango cha lami mpaka Ruaha
National Park ili kuongeza mapato ya nchi lakini pia kuongeza vipato kwa
wananchi wa barabara hii wanayoitumia”.
“Kwa
faida hizo nimeamua mimi mwenyewe kuvunja leo hii nyumba ili wananchi
wa eneo hili ambao barabara hii itajengwa lazima wahakikishe wanabomoa
wenyewe nyumba zao,” alisema Waziri Lukuvi.
Aidha
Waziri Lukuvi aliwataka wananchi wote waliojenga ndani ya eneo la
hifadhi ya barabara kuzivunja wenyewe nyumba zao ili kurahisisha zoezi
la upanuzi wa barabara hiyo uwe wa muda mfupi, kwani barabara hiyo
inajengwa kwa manufaa yao.
“Lazima
tutii sheria bila shuruti. Tuliowekewa alama ya X tuvunje nyumbza zetu
ili kazi ya ujenzi wa barabara hii iwe nyepesi, gharama iwe ndogo na
iende kwa muda mfupi,” alisema Waziri.
Vilevile
aliwakumbusha wakazi wa eneo hilo ambao wamejenga ndani ya eneo la
hifadhi ya barabara kuwa wasitegemee fidia yoyote kutoka serikalini na
badala yakee waanze kuzibomoa nyumba zao pasipo kusubiri kuja kubomolewa
kwa nguvu.
“Serikali haitolipafidia kabisa kwa watu waliojenga kwenye eneo la barabara kama mimi,” alisema.
0 comments: