Mbunge
wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe
amefunguka na kusema kuwa serikali ya awamu ya tano inadhamira ya kuuwa
vyama vya upinzani nchini kwa muswada wa sheria ambao umesambazwa kwenye
vyama vya siasa.
Zitto
Kabwe anasema muswada huo ambao umesambazwa tayari kwa vyama vya siasa
ni kama hukumu ya kuviuwa vyama vya upinzania nchini kwani kuna vifungu
ambavyo vinakataza vyama vya siasa kisheria kufanya mikutano ya hadhara
isipokuwa mwaka wa uchaguzi tu, lakini pia watu wanaoruhusiwa kufanya
mikutano hiyo ni wabunge na madiwani tu kwenye majimbo yao husika.
Kufuatia
jambo hilo Zitto Kabwe amesema kuwa hawatakubali jambo hilo na
watapinga sheria hiyo ndani ya Bunge pamoja na nje ya bunge na kusema
wao watalinda mfumo wa vyama vingi nchini kwa gharama yoyote kwani uwepo
wa vyama ni haki Kikatiba.
0 comments: