Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imetekeleza amri za
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kumpeleka mshtakiwa katika kesi ya
uhujumu uchumi, Harbinder Sethi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Mwendesha
Mashtaka Mwandamizi wa Takukuru, Leonard Swai leo Ijumaa amemweleza
Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa wametekeleza amri za Mahakama
walizopewa kwa kumpeleka Sethi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
kwamba kinachosubiriwa ni ripoti ya daktari.
Swai
ameeleza kutokana na hali hiyo, Sethi atarudishwa katika hospitali hiyo
kwa ajili ya kuchukua majibu ya vipimo vyake wiki ijayo.
Baada
ya maelezo hayo wakili wa mshtakiwa, James Rugemalira, Respicius Didas
ameeleza mahakamani hapo kuwa kuna suala la ucheleweshwaji wa upelelezi
na kwamba washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo Juni 19,mwaka 2017
na wapo ndani hadi sasa.
Wakili
Didas ameeleza kuwa upande wa mashtaka unawaambia upelelezi bado
haujakamilika, wateja wao wanaendelea kukaa ndani na kwamba kuna athari
sana.
Akijibu
hoja hiyo, Swai amesema kuwa uchunguzi wa kesi ya kughushi unachukua
muda hivyo aliomba mawakili wa upande wa utetezi wajue upelelezi bado
unaendelea na kwamba sheria ipo wazi katika masuala ya kughushi.
Hakimu
Shaidi yeye aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 27,2017 ambapo kesi
hiyo itatajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Katika
kesi hiyo, washtakiwa Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12
ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu,
kighushi, kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia za
udanganyifu.
Pia wanakabiliwa na mashtaka matano ya kutakatisha fedha pamoja na kusababisha hasara ya Sh 309.4 bilioni
0 comments: