Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO), linawataarifu Wateja wake kuwa Jumamosi
Novemba 18 na leo Jumapili Novemba 19, 2017 kuna usafishaji na kuunga
bomba kubwa la Gesi katika Mitambo ya Kinyerezi I, sambamba na zoezi
hilo pia yanafanyika maandalizi ya kukiunganisha Kituo cha Kinyerezi II,
kuanzia Saa:02.00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni, kama tulivyowatangazia.
Kutokana
na kazi hiyo kutakuwa na upungufu wa umeme katika Gridi ya Taifa, hivyo
baadhi ya Wateja waliounganishwa katika Gridi ya Taifa wa maeneo
mbalimbali Nchini watakosa huduma ya umeme.
Zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi mkubwa na uharaka ili kurejesha huduma ya umeme kwa wakati.
TAHADHARI
Kutokana
na kazi hii Wananchi mnaombwa msipite karibu na eneo la Mitambo ya
Kinyerezi, kutokuwasha moto, kutokufanya shughuli za uchomeleaji vyuma
pamoja na shughuli nyingine yoyote yenye viashiria vya moto, ili
kujikinga na madhara yanayoweza kutokea iwapo shughuli tajwa zinafanyika
maeneo yaliyo karibu na Mitambo.
Shirika limesha fanya taratibu zote za ki usalama katika eneo la Mitambo.
0 comments: