Ukisikia Kakobe amezungumza, tafakari kwanza kabla ya kumkabili


Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe amejibu hoja zinazotolewa dhidi yake, baadhi zikitolewqa na Serikali akisema anapozungumza ni lazima kutafakari kabla ya kumkabili.

Askofu Kakobe alizungumza jana wakati wa ibada katika kanisa la FGBF lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

“Ukisikia Kakobe amezungumza, tafakari kwanza kabla ya kumkabili,” alisema.

Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni siku moja baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutangaza kuanzakufuatilia ulipaji wake wa kodi.

Uamuzi wa TRAulitangazwa juzi na Kamishna Mkuu, Charles Kichere mbele ya waandishi wa habari baada ya hivi karibuni Askofu Kakobe kusikika akisema ana fedha nyingi kuliko Serikali.

TRA ilisema uamuzi huo unatokana na kiongozi huyo wa kiroho kutokuwemo katika kumbukumbu za ulipaji kodi za mamlaka hiyo. Mamlaka hiyo ilisema kama utajiri wake unatokana na sadaka pekee litakuwa jambo la kushtua.

Jana, Askofu Kakobe alitumia ibada hiyo kuwajibu TRA na pia alizungumzia mambo mengine mawili; uraia wake na onyo la Serikali la kuwataka viongozi wa dini kutokuzungumzia masuala ya siasa.

“Tangu nilipoitika wito huu miaka 30 iliyopita, sijawahi kufanya biashara yoyote zaidi ya hii na kanisa hili halina mradi wowote wa kiuchumi. Kakobe hana mradi wowote na kama yupo anayejua ajitokeze aseme nitampa zawadi,” alisema Askofu Kakobe.

“Akaunti yetu iko Benki ya NBC na iko chini ya Bodi ya Wadhamini, bodi ambayo imesajiliwa Rita (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini). Kwa hiyo, hao wanaotaka kujua zaidi waende Rita wakaulize wajumbe wa bodi hii ni akina nani na waende NBC kuona vyanzo vyetu vya mapato kama ni tofauti na sadaka.”

Huku akishangiliwa na waumini, alisema tatizo kubwa lililojitokeza nchini ni watu kutafasiri wanavyojua na kujikuta wakipotoka. Alisema hilo ni tatizo watu kutopenda kusoma Biblia kwa undani na kwa upana zaidi.

“Wamemsikia Kakobe anazungumza hapa, anazungumza mambo ya rohoni kuhusu haya ya utajiri. Unaweza kusikia maneno ukatafsiri kivyako kwa sababu haya tunayozungumza hapa ni mambo ya rohoni, wewe unayatafsiri kisiasa,” alisema Kakobe.

“Wanasema wewe una hela kweli kuliko Tanzania sema... ninaweza kuvunja hekalu na kulisimamisha kwa siku tatu. Mtu anajiuliza hekalu gani hili? Hekalu hili ni mwili wake. Maana yake niueni, nisulubisheni, lakini nitakufa na siku ya tatu nitafufuka, hii ndio hekalu, unatafsiri kwa akili.”

Kwa sauti ya juu na yenye msisitizo, Askofu Kakobe alisema: “Kimsingi, mimi si mtu tu tajiri kuliko Serikali, bali ni tajiri kuliko Serikali zote duniani. Kwa hiyo ukisikia Kakobe amezungumza, tafakari kwanza kabla ya kumkabili.”

“Hela yote ya Serikali ya Tanzania au dunia nzima haiwezi kununua tiketi hata moja ya Mbinguni. Mimi ni tajiri kuliko Serikali ya Magufuli (Rais John Magufuli) au Serikali ya Trump (Rais wa Marekani Donald Trump),” alisema.

Alisema nyumba anayoishi iliyopo Kijitonyama karibu na Kituo cha Polisi Mabatini jijini Dar es Salaam aliijenga miaka ya sabini na tangu wakati huo hajawahi kujenga kokote na gari lake ni la kawaida.

Askofu Kakobe alisema maisha yake si ya kifahari kama wasemavyo watu.

Uraia wake
Kuhusu uraia, Askofu Kakobe alisema wazazi wake walikuwa wakiishi Kakonko mkoani Kigoma na baada ya kufariki walizikwa huko, huku uraia wake ukifuatiliwa na ilibainika ni raia halali.

“Baba yangu alikuwa mwalimu kwa kipindi kirefu, amefanya kazi Tanga, Sumbawanga, Usukumani kwa Wanyamwezi, Tabora na Shinyanga. Miongoni mwa watu tuliocheza pamoja katika utoto wetu ni Christopher Chiza, huyu alikuwa waziri,” alisema Kakobe.

“Ukitaja kwa jumla familia yetu, inajulikana miaka mingi. Walikwenda kuchunguza uraia wangu na kujiridhisha pasina shaka na kusema huyu ni Mtanzania. Kuna kipindi watu walikwenda mara tatu kijijini kwangu Kakonko kuchunguza uraia.”

Waumini wakiwa kimya wakimsikiliza, Askofu Kakobe alisema, ‘’ Nimezaliwa Tanzania, wazazi wangu wamezaliwa Tanzania, mimi ni Mtanzania kwa hiyo sitoki hapa, tutabanana hapa hana.”

“Baada ya kuona, yote hayo, mara waende huku, waende huko waulize wazazi wangu ambao wamefariki hivi karibuni na makaburi yapo kijijini na niliwaambia makaburi wayaweke barabarani ili anayechunguza uraia wangu aanzie pale,” alisema.

Alisema, ‘’Kila jambo chini ya mbingu kuna kusudi, kuna kusudi la Mungu mimi kuzaliwa Tanzania, kwa hiyo wanaosema nimetoroka hawanisumbui kichwa.”

Kuhusu taarifa za kutoroka nchini alisema: “Ninapokwenda na kurudi washirika wa hapa wanajua. Kwa mfano safari ya mwisho ilikuwa Agosti (mwaka jana) na tangu hapo sijasafiri. Niko hapa na haya mengine nayasikia nimetoroka, hayanisumbui, ukiitwa majina si yako unasumbukia nini?”

1 comments:

Chadema Yawataka Viongozi Wa Dini Kuendelea Kuikosoa Serikali



Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amewataka Watanzania kuwa tayari kukosolewa na viongozi wa dini kwani ndio wanaoliombea Taifa liwe na amani katika kipindi chote tangu nchi ilipopata Uhuru.

Mbowe ameyasema hayo jana wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu hali ya kisiasa kwa mwaka 2017, ambapo alisema kila mtu ana mapungufu katika utendaji wake wa kazi hivyo kila mmoja awe tayari kupokea ushauri kutoka kwa viongozi wa dini.

“Lakini viongozi wetu wa dini wana haki ya kusema, wana wajibu wa kusema, hawa ni watu wanaolea Taifa hili kiroho, huwezi kumshambulia Kakobe kama unamshambulia mtoto mdogo, hawa wana waumini wana followers (wafuasi) na hawa ndio kila siku Rais anasema wamwombee, sasa wanamwombea vipi wakati unawapa masharti?,” alisema Mbowe na kuongeza.

“Sisi wapinzani tunakosolewa, viongozi tuwe na unyenyekevu wa kukubali mawazo tofauti tukisemwa, tusijenge chuki katika jamii, vyama vyetu vyote vinaongozwa na binadamu vinaweza vikakosea, tuwaache viongozi wa dini wafanye kazi yao, tukikosea waseme.”

0 comments:

Lipumba ataka mjadala wa kitaifa kuhusu uchumi


Mtaalamu wa Uchumi, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu uchumi na mustakabali wa Taifa.

Profesa Lipumba ameyasema hayo jana Jumapili Desemba 31,2017 wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam kujadili hali ya uchumi kwa mwaka 2017.

Alisema kuna haja ya kujadili sera za kiuchumi, namna ya kujenga uchumi unaoongeza ajira kwa wananchi na kutafuta suluhisho la matatizo yanayowakabili Watanzania.

“Tuitishe mjadala wa kitaifa tuje kujadili, tutazame upya sera za kiuchumi, namna ya kujenga uchumi unaoongeza ajira utakaoleta manufaa kwa wananchi wote. Tujadili kimsingi na tutoke na sera ambazo tunaweza kuishauri Serikali nini cha kufanya,” alisema Profesa Lipumba.

Katika mjadala huo, Profesa Lipumba alisema Serikali haiwezi kufanikisha mapinduzi ya viwanda kama haijafanikisha ya kilimo kwa sababu ukuaji wa kilimo ndiyo ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi.

Alisema robo tatu ya Watanzania wanategemea kilimo lakini ukuaji wa sekta hiyo ni mdogo kutokana na Serikali kukiacha nyuma kilimo na kukumbatia sekta nyingine.

Profesa Lipumba alisema kuna changamoto kubwa kwenye kilimo ambazo zinatokana na ukweli kwamba, Serikali haijawekeza vya kutosha kwenye utafiti wa kilimo, mafunzo kwa wakulima na usambazaji wa pembejeo.

“Tujifunze kwa nchi za Asia kama vile China, India na Malaysia, wao wamewekeza kwa wakulima wadogowadogo,” alisema Profesa Lipumba.

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeshiriki mjadala huo, alisema mfumo wa elimu wa sasa wa Tanzania unamwandaa mtu kuwa tegemezi badala ya kujitegemea kama ilivyokuwa zamani.

Alisema kuna umuhimu wa kufumuliwa upya kwa mfumo huo tegemezi ili kujenga utakaowafanya vijana wajifunze kujitegemea au ujasiriamali.

Bashe alisema Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa idadi kubwa ya mifugo lakini hakuna dira ya wazi ni wapi pajengwe viwanda.

Akichangia mada ya hali ya uchumi, mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU), Dk Bravious Kahyoza alisema Tanzania haijazalisha ajira za kutosha kwa wananchi kwa sababu ya kusinyaa kwa uchumi.

Alisema Serikali imekuwa ikishindana kukopa na sekta binafsi jambo lililosababisha sekta binafsi kubaki nyuma na kushindwa kuajiri watu wengi kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi.

lietaka kuwepo uwiano kati ya sera za kifedha na zile za kibajeti ili kuleta matokeo mazuri kwenye uchumi.

“Wataalamu wetu wanapaswa kukaa chini na kuangalia kama tuko kwenye njia sahihi kuelekea mpango wa maendeleo wa miaka mitano na uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025. Kama hatuko sahihi basi ni vyema tukabadilisha mbinu tunazotumia kufika huko,” alisema.

0 comments:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya January 1 , 2018.....Ni Mwaka Mpya !....


0 comments:

DK SHIKA ATANGAZA KUIHAMA TANZANIA


Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kuishi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo.


Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani.


“Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu halafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa Bara la Afrika, sasa ni world wide, ofisi itakuwa New York, nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR.


“Hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, hizi ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina langu lilikuwa projected na Urusi na mwenyewe Rais Vladimir Putin”, amesema Dkt. Shika.


Dkt. Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina lake kupitishwa ikiwemo na Marekani

0 comments:

BREAKING: Serikali Imetoa Tamko Kuhusu Matumiizi ya Fedha za Kigeni Hapa Nchini


Seebait.com 2017
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo kuhusu matumizi ya fedha za kigeni katika  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusisitiza kuwa utekelezaji wake uanze  tarehe 1 Januari, 2018.  Maagizo hayo ni kama ifuatavyo: –
  1. Bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi ya nyumba za kuishi na maofisi, bei ya ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya kielektroniki.
  2. Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza kufanyika kwa fedha za kigeni. Bei hizi zinajumuisha gharama za usafirishaji kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za nje, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa wageni, na gharama za hoteli kwa watalii kutoka nje ya nchi. Walipaji wanaotumia fedha za kigeni watambuliwe kwa vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa makampuni.
  3. Viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na visizidi vile vya soko. Ifahamike wazi kuwa ni mabenki na maduka ya fedha za kigeni tu yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.
  4. Mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yeyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.
Aidha Dkt. Mpango ameviagiza vyombo vya dola viwachukulie hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo haya ya Serikali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

0 comments:

Kanusho la taarifa inayosambazwa kumuhusu Makamu wa Rais


Seebait.com 2017SeeBait
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii linalomhusisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kuwa atashiriki zoezi la kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya tarehe 1-1-2018. 

Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la kweli na Makamu wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho kwa tarehe iliyotajwa.

Ikumbukwe kuwa siku ya tarehe 15-12-2017 wakati wa hafla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza kampeni ya kupanda miti Dodoma ambayo itaratibiwa na Ofisi yake .

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzingatia matangazo, taarifa na ratiba zitakazotolewa na Ofisi yake kuhusu programu ya upandaji miti Dodoma.

 Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma

 30 Desemba, 2017.

0 comments:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba



0 comments: