*KIVULI CHA DAVIS MOSHA CHAMTESA BOISAFI*
Nipo Moshi likizo, Bado likizo yangu ni ndefu mpaka January ndio narudi kutafuta Dar es salaam, Kila December tunarudi Home kuhesabiwa, Moshi kumechangamka sana, Moshi ya sasa sio ile ya zamani, Huku kila mmoja anaongelea Maendeleo Ya Moshi. Nipo huku Moshi nakutana na Mchakato wa Uchaguzi wa CCM Wilaya na Mkoa katika Jumuhia zake. Nimejikuta nikifuatilia kwa Ukaribu sana. Kitu kikichonivutia ni Duru la Uchaguzi wa Jumuhia ya Wazazi na Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa.
Katika Uchaguzi wa wazazi nimeona Wazee wameamua kubadili Upepo, Upepo wa kumuamini kijana Mdogo aweze kuwaongoza, Huyu kijana anaitwa Mrindoko, Nilijikuta nahitaji kumfahamu zaidi japo sikufanikiwa kukutana nae. Cha Ajabu ni kuwa nasikia huyu kijana Jina lake limepitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM.
Katika Nafasi hiyo yupo Mfanyabiashara Maarufu *Boisafi* Huyu mfanyabiashara aliwahi kugombea uteuzi wa nafasi ya Ubunge katika chama akashindwa na Mfanyabiashara *Davis Mosha. Leo amerudi anataka kuwa Boss wa Mkoa wa Kilimanjaro katika Chama. Kwa upande wangu naona *This is project* huu ni Mradi wa wafanyabiashara wachache kumiliki chama. Najiuliza Maswali Machache, Hivi huyu Boisafi si ndiye alisusia Uchaguzi wa CCM baada ya kushindwa kwenye Kura za Maoni? Huyu Boisafi si ndiye aliyekua akihakikisha Mgombea ubunge wa CCM anashindwa uchaguzi sababu tu alimshinda kura za Maoni?
Kama aliweza Kumdharau hata Katibu Mkuu alipomwambia Avunje Makundi baada ya Kura za Maoni atashindwa kukudharau wewe Katibu wa Tawi?
Huku Moshi zipo Tetesi kuwa Yeye na Team yake ndio walipendekeza jina la Meya wa Chadema na likapitishwa. Leo anataka Unyekiti wa Mkoa? Inabidi Ifike Mahali CCM iwatazame wagombea wake wanaowapitisha katika nafasi nyeti kwa jicho la tatu, *BOISAFI ANAGOMBEA?* Sitaki kuwasemea wagombea wengine ila hii haina Afya kabisa kwa Chama. Mimi napenda Siasa, Naipenda CCM kutoka Moyoni ila kwa hili tuna safari ndefu katika kukomboa Majimbo ya Mkoa wa Kilimanjaro yaliyopotea.
Nasikia Hata Uchaguzi Mdogo wa Udiwani huyo *Boisafi* Hakushiriki sasa anataka hiyo nafasi ya nini? *CCM msikubali huu mradi wa Matajiri wachache*
Kichekesho kikubwa wanasema *Davis Mosha Kampa huyo Mrindoko Pesa ili agombee Uwenyekiti, Hivi *Davis* si aliacha Siasa? Si aliaga wananchi wa Moshi mjini? Na Mwenyekiti wa Mkoa anamzuia nini Davis kugombea kama akihitaji tena?
Kweli Kivuli cha *Davis Mosha* Kinamtesa Boisafi. *Davis* na Boisafi ni wanachama wa CCM wote wapo katika daraja Moja katika chama tofauti yao ni Uzalendo tu. Mmoja sio mzalendo yupo tayari kusaidia Adui ili aridhishe nafsi yake Mwingine ni Mzalendo hawezi msaidia Adui katika Chama ambaye anapigana na chama.
J.S. MUSHI
*CCM KILIMANJARO MNAHITAJI TAFAKURU YA UHAKIKA*
About author: PAVEA BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: