Bilionea
Mohammed Dewji ameipokea kwa mikono miwili ishu yake ya ushindi kuwa
mwekezaji mpya Simba na ametoa ahadi zake 10 kuhakikisha zinafanyika
kuleta mabadiliko makubwa.
Mo
Dewji ameshinda zabuni ya kuwa mwekezaji wa Simba kwa dau la Sh bilioni
20 alizoweka ‘mezani’ na hakukuwa na mtu yoyote aliyejitokeza
kushindana naye kama ilivyokuwa ikielezwa awali.
MOJA:
Kambi
ya Simba itajengwa upya kabisa na itakuwa ni hosteli ya kisasa yenye
vyumba hadi 35. 30 vitakuwa kwa ajili ya wachezaji na vitano kwa ajili
ya benchi la ufundi.
MBILI:
Simba
sasa itafaidika kwa kuwa na gym yake ya kisasa, bwawa kubwa la kuogelea
kwa ajili ya mazoezi na sehemu ya kupumzika kwa wachezaji.
TATU:
Wachezaji, makocha na viongozi watakuwa na mgahawa wao wa kisasa kabisa.
NNE:
Mo
Dewji anaamini timu lazima iwe na viwanja vya mazoezi. Hivyo ataanza na
viwanja viwili, kimoja nyasi asilia na kingine nyasi bandia.
TANO:
Mo Dewji ameahidi kuwekeza katika soka la vijana akianza na wale wenye umri wa chini ya miaka 14, 16 na 18 na lengo ni kuwakuza.
SITA:
Mo Dewji amesema atasimamia wachezaji kuitambua thamani ya Simba kwa kujituma hasa.
SABA:
Simba
itaanza kufanya mambo kimataifa kwa kuitangaza na kuikuza brand ikiwa
ni pamoja na kutengeneza vifaa mbalimbali kama fulana, kofia, vishika
ufunguo na kadhalika.
NANE:
Ameahidi
kutenga kitita cha Sh milioni 500 ambazo zitatumiwa na benchi la
ufundi katika mipango yao kama kambi na kadhalika pia Sh bilioni moja
kwa ajili ya usajili.
TISA:
Kushindana na timu kubwa Afrika na sio Tanzania pekee.
KUMI:
Kurejesha Simba katika historia ya kimataifa
0 comments: